Habari RFI-Ki-logo

Habari RFI-Ki

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Felix Tshisekedi atangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais DRC

1/9/2019
More
Katika makala haya utasikia maoni ya wachangiaji kuhusu ushindi wa Felix Tshisekedi katika nafasi ya Urais nchini DRC

Duration:00:09:59

Mpango wa umoja wa Afrika kupunguza kikosi cha AMISOM nchini Somalia una tija?

12/20/2018
More
Umoja wa Afrika AU unapanga kupunguza wanajeshi 1000 waliopo katika kikosi cha kulinda amani cha AMISOM nchini Somalia. Hata hivyo hatua hii inachukuliwa huku bado taifa hilo la pembe ya Afrika likikabiliwa na changamoto za usalama. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao

Duration:00:10:13

Uchaguzi wa DRC wapigwa kalenda, wananchi watoa maoni yao

12/19/2018
More
Kuna ripoti kuwa uchaguzi wa DRC huenda ukaahirishwa kutokana na changamoto mbalimbali huku baadhi ya maeneo kampeni zikipigwa marufuku. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni yao.

Duration:00:09:54

Dunia yaadhimisha siku ya haki za binadamu, huku nchi za Afrika mashariki zikikabiliwa na changamoto za kuheshimu haki za binadamu

12/9/2018
More
Disemba 10 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya haki za binadamu lakini bado mataifa ya Afrika mashariki yanakabiliwa na changamoto za kusheshimu haki za binadamu. fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:09:39

Serikali ya Kenya yasisitiza wanafunzi waliopata ujauzito wataruhusiwa kuendelea na elimu ya sekondari

12/4/2018
More
Serikali ya Kenya kupitia wizara ya elimu imesisitiza kuwa wanafunzi waliopata ujauzito wataruhusiwa kuendelea na elimu ya sekondari mwaka 2019. Je hatua hii ina maana gani na ikiwa inafaa kuigwa na mataifa mengine? Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji kupata maoni yao

Duration:00:09:33

Changamoto za wavuvi katika maeneo ya maji katika nchi za maziwa makuu zinafanyiwa kazi?

11/22/2018
More
Makala haya inaangazia changamoto zinazowakabili wavuvi katika eneo la maziwa makuu. Je mamlaka zinachukua hatua gani? Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:09:45

Raia wa DRC wazungumzia kampeni za uchaguzi nchini mwao

11/21/2018
More
Kampeni za uchaguzi mkuu wa DRC zimeng'oa nanga kwa wagombea kuanza kunadi sera zao. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kukusanya maoni ya raia wa DRC kuhusu namna wanavyoshuhudia kampeni katika maeneo yao.

Duration:00:09:51

Ulimwengu unaadhimisha siku ya televisheni

11/20/2018
More
Dunia inaadhimisha siku ya televisheni inayotajwa kusaidia maendeleo na ukuaji wa haki za binadamu. Je msikilizaji Luninga imekusaidia nini? Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya.

Duration:00:10:09

Dunia yaathimisha siku ya kimataifa ya mtoto huku kundi hilo likikabiliwa na changamoto lukuki

11/19/2018
More
Novemba 20 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya mtoto huku barani Afrika watoto wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa lishe bora, ukosefu wa elimu na usalama. Je jamii inatimiza wajibu wake katika kukuza ustawi wa mtoto? Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya.

Duration:00:09:57

Matarajio ya wananchi wa DRC, wakati huu wagombea wakitarajia kuanza kunadi sera zao

11/18/2018
More
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini DRC zinatazamiwa kuanza wiki lakini yapi ni matarajio ya raia wa DRC kwa wagombea wa nafasi mbalimbali. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:10:07

Mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko DRC yanatoa taswira gani wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi?

11/15/2018
More
Askari saba, sita kutoka Malawi na mmoja kutoka Tanzania wameuawa katika Mji wa Beni, Mashariki mwa DRC. Je matukio haya ya mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanatoa taswira gani wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi? Fredrick Nwaka ameakuandalia makala ya Habari Rafiki kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:10:02

Eritrea yaondolewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

11/14/2018
More
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeondolea vikwazo taifa la Eritrea ambavyo vilikuwa vimedumu kwa karibu muongo mmoja. Vikwazo hivyo zilihusisha marufuku ya ununuzi wa silaha na mengineyo. Je uamuzi wa UN una maana gani katika kuleta utulivu katika eneo la pembe ya Afrika, Fredrick Nwaka amekuandalia makala ya Habari Rafiki kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:10:17

Sudani Kusini kusherehekea Mkataba wa amani huku raia wake wakikabiliwa na changamoto lukuki

10/29/2018
More
Nchi ya Sudani Kusini kesho itafanya sherehe ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani ambayo lengo lake ni kuthitisha vita. Hata hivyo hafla hii inakuja hguku taifa hilo changa duniani likikabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo za usalama, ukosefu wa chakulam mauaji n.k. Fredrick Nwaka ameandaa makala ya Habari Rafiki kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

Duration:00:09:52

Kusuasua kwa mkakati wa kusaka amani nchini Burundi

10/28/2018
More
Awamu ya tano ya mazungumzo ya kusaka amani ya Burundi imetamatika huko Arusha nchini Tanzania huku serikali ikisusia mazungumzo hayo. Mwezeshaji wa mazungumzo hayo na rais Mstaafu wa tanzania, Benjamin Mkapa amearifu kuwa atapeleka mapendekezo ya wanasiasa wa upinzani kwa wakuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki. Je Mapendekezo ya wanasiasa wa upinzani yatakuwa na tija ikiwa serikali ilisusia mazungumzo hayo. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao

Duration:00:10:06

Bunge la AU laangazia mapambano dhidi ya ufisadi

10/21/2018
More
Bunge la Afrika AU limeendelea na vikao vyake mjini Kigali nchini Rwanda ambapo suala la ufisadi likiwa ajenda kuu ya vikao.Wasikilizaji wanaangazia jitihada za serikali kutekeleza azma ya kukomesha ufisadi,.

Duration:00:10:29

Serikali za Afrika Mashariki na Kati zinachukua hatua gani kukabiliana na visa vya raia wake kushambuliwa katika mataifa ya Arabuni?

10/18/2018
More
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati miezi ya karibuni yameripoti visa vya raia wake kushambuliwa na hata kuuliwa katika mataifa ya Asia.Serikali za Afrika Mashariki na Kati zinachukua hatua zipi kulinda raia wake wanaokwenda kutafuta ajira barani Asia. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni.

Duration:00:10:02

Serikali ya burundi yasitisha shughuli za mashirika ya kimataifa

9/27/2018
More
Serikali ya burundi imezua gumzo baada ya kusitisha shughuli za mashirika ya kiraia nchini humo kwa kile ilichosema inachunguza ikiwa yanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.

Duration:00:09:27

Mauaji ya Beni yawachosha raia wa mashariki mwa DRC

9/25/2018
More
Jeshi la DRC (FARDC) limeshtumu muungano unaojumuisha raia wa kigeni "wanaoendesha harakati zao kutoka nchi jirani" kuhusika katika mauaji ya mara kwa mara katika eneo la Beni, Mashariki mwa nchi hiyo.

Duration:00:09:26

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa 73 una umuhimu gani kwa Waafrika

9/24/2018
More
Mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja wa Mataifa ambao ulianza tangu Jumanne wiki hii huko New York nchini Marekani umeendelea kugubikwa na mvutano na hotuba za kushtumiana kati ya baadhi ya viongozi wa nchi.

Duration:00:10:07

Changamoto za Udhibiti wa ajali za majini waangaziwa baada ya ajali ziwani Victoria Tanzania

9/23/2018
More
Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake kutoka Bugorola kwenda Ukara Mwanza nchini Tanzania kilizama Septemba 20 kikiwa na zaidi ya watu 250 na kufikia leo juhudi za uokozi zimefanikiwa kuokoa watu 41 na kuopoa miili 227.

Duration:00:10:20