Jukwaa la Michezo-logo

Jukwaa la Michezo

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Hatima ya fainali za Afrika mwaka 2019 baada ya Cameroon kupokwa uenyeji

12/1/2018
More
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la kandanda Afrika CAF wiki hii ilitangaza kuipoka Cameroon uenyeji wa fainali za 32 za michuano hiyo zilizopangwa kufanyika Juni hadi Julai mwaka 2019. Ipi itakuwa hatima ya mashindano hayo makubwa ya kandanda barani Afrika? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Aloyce Mchunga na Boniface Osano kutathimini kwa kina.

Duration:00:20:25

Dhamira ya George Weah kulipa mishahara ya wachezaji wa Timu ya Taifa inaweza kuigwa na mataifa mengine ya Afrika?

11/24/2018
More
Rais wa Liberia, George Opong Weah ametangaza kuwa serikali yake inakusudia kuanza kuwalipa mishahara wachezaji wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Je hatua hii inaweza kuongeza hamasa na hata kuigwa na mataifa mengine ya Afrika? Fredrick Nwaka ameungna na mchambuzi wa soka Aloyce Mchunga kukuletea makala haya.

Duration:00:19:02

Tanzania yaweka rehani matumaini ya kufuzu Afcon huku Ghana ikichanua

11/17/2018
More
Tanzania imeshindwa na Lesotho kwa bao 1-0 na kuweka rehani matumaini ya kufuzu fainali za Afrika huku Ghana, Kenya, DRC zikiweka hai matumaini yao. Ungana na Fredrick Nwaka na Victor Abuso wakitathimini kwa kina

Duration:00:20:25

Nafasi ya klabu za Afrika Mashariki na Kati katika michuano ya klabu, Afrika mwaka 2018/2019

11/10/2018
More
Shirikisho la kandanda Afrika, CAF limetoa droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika ni ile ya taji la Shirikisho. Je ipi nafasi ya klabu kutoka Afrika Mashariki na Kati kufua dafu katika michuano hiyo? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Aloyce Mchunga na Boniface Osano kutathimini kwa kina

Duration:00:21:16

Simba SC yapata viongozi wapya na Michuano ya klabu Afrika, kuanza Novemba 2018

11/3/2018
More
Klabu ya Simba imefanya uchaguzi wa viongozi wapya watakaoiongoza kwa miaka minne na msimu wa michuano ya ngazi ya klabu Afrika kuanza Novemba mwaka 2018. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samwel John na Boniface Osano kuangazia kwa kina.

Duration:00:23:44

Kusuasua kwa mkakati wa kusaka amani nchini Burundi

10/28/2018
More
Awamu ya tano ya mazungumzo ya kusaka amani ya Burundi imetamatika huko Arusha nchini Tanzania huku serikali ikisusia mazungumzo hayo. Mwezeshaji wa mazungumzo hayo na rais Mstaafu wa tanzania, Benjamin Mkapa amearifu kuwa atapeleka mapendekezo ya wanasiasa wa upinzani kwa wakuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki. Je Mapendekezo ya wanasiasa wa upinzani yatakuwa na tija ikiwa serikali ilisusia mazungumzo hayo. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao

Duration:00:10:06

Mkutano wa baraza la nane la Fifa wamalizika Kigali, nchini Rwanda

10/27/2018
More
Mkutano wa nane wa baraza la Utendaji la Shirikisho la Kandanda duniani Fifa umetamatika nchini Rwanda wiki hii kwa maazimio mbalimbali kupitishwa. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Boniface Osano na Samwel John kutathimini kwa kina

Duration:00:21:08

Kenya iko tayari kushiriki fainali za Afrika za Wanawake nchini Ghana?

10/20/2018
More
Kenya imepata nafasi ya kushiriki fainali za Afrika kwa wanawake baada ya Rquatorial Guinea iliyokuwa imefuzu kuondolewa baada ya kubainika kutumia wachezaji wasio raia wa nchi hiyo. Je Kenya iko tayari kwa fainali hizo zinazotazamiwa kuanza Novemba 17 hadi Disemba 1. Fredrick Nwaka ameungana na Naibu rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF Doris Petra na Mchambuzi wa Soka Samwel John kutathimini kwa kina.

Duration:00:21:31

Michuano muhimu ya kuwania kufuzu fainali za Afrika yarindima

10/13/2018
More
Mechi za kuwania kufuzu fainali za Afrika za mwaka 2019 nchini Cameroon zimeendelea tena wikendi hii. Tanzania ikipoteza mbele ya Cape Verde, wakati Kenya ikipata sare mbele ya Ethiopia. Victor Abuso na Fredrick Nwaka wanajadili kwa kina

Duration:00:24:15

Cameroon yasema iko tayari kuandaa fainali za Afrika mwaka 2019

10/6/2018
More
Serikali ya Cameroon imesema iko tayari kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2019 licha ya kukabiliwa na changamoto za miundombinu. Victor Abuso ameungana na Fredrick Nwaka kukuletea uchambuzi wa kina kuhusu hili na matukio mengine ya kimichezo.

Duration:00:21:03

Watani wa jadi Simba na Yanga washindwa kufungana

9/29/2018
More
Watani wa jadi katika mchezo wa soka nchini Tanzania Simba na Yanga walishindwa kufungana katika mchezo muhimu wa ligi kuu, Tanzania bara. Tunajadili mechi hii kwa undani namna ilivyokuwa.

Duration:00:23:16

Ligi ya Tanzania bila mdhamini

9/22/2018
More
Tuynatathimini kuanza kwa ligi ya Tanzania bila mdhamini mkuu.Karibu

Duration:00:21:45

Mechi za robo fainali ya taji la klabu bingwa Afrika na taji la shirikisho zarindima

9/15/2018
More
Mechi za hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika na zile za taji la shirikisho zimekuwwa zikichezwa wikendi hii. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samwel John na Boniface Osano kuangazia kwa kina.

Duration:00:22:13

Mataifa ya Afrika yaendeleza mapambano ya kufuzu AFCON 2019

9/8/2018
More
Mwishoni mwa wiki hii, mataifa mbalimbali ya Afrika yapo viwanjani kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza fainali ya soka kuwania ubingwa wa Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon. Tunakuletea uchambuzi wa kina.

Duration:00:23:41

Mwelekeo wa soka la Afrika Mashariki na kati baada ya Kenya kujiondoa kuandaa michuano ya Cecafa

9/1/2018
More
Shirikisho la kandanda nchini Kenya, FKF Nick Mwendwa amearifu uamuzi wa shirikisho la soka nchini Kenya kujiondoa kuandaa michuano ya Cecafa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Je uamuzi huu una maana gani kwa soka la Afrika Mashariki na Kati? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samwel John na Austin Oduor Otineo kutathimini suala hili.

Duration:00:20:52

Mwelekeo wa soka la vijana Afrika Mashariki na kati baada ya kutamatika kwa michuano ya kufuzu fainali za Afrika Jijini Dar es salaam

8/25/2018
More
Michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, kanda ya Afrika Mashariki na Kati zimefikia tamati Jijini Dar es salaam, Tanzania kwa Uganda kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ethiopia na kuungana na Tanzania kucheza fainali zitakazochezwa mwaka 2019 nchini Tanzania. Je uamuzi wa kuchezwa mechi za mchujo katika kanda ulikuwa sahihi na nini hatima ya soka la vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samuel John na Ali Saleh...

Duration:00:23:58

Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kuanza Agosti 22 bila mdhamini mkuu

8/18/2018
More
Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2018/19 itaanza Agosti 22 ikishirikisha timu 20. Mamlaka inayosimamia ligi, Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imesema ligi hiyo itaanza bila kuwepo kwa kwa mdhamini mkuu. Fredrick Nwaka ameungana na mtendaji mkuu wa Azam FC Abdulkarim Amim na mchambuzi wa soka Samwel John kutathimini kwa kina.

Duration:00:24:16

Mechi za kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, zaanza nchini Tanzania

8/11/2018
More
Shirikisho la soka Afrika CAF kubadili mfumo wa mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, una tija? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Juma Mudimi na Abdulsuleimani Semugenyi

Duration:00:22:13

Kenya ndio bingwa wa mashindano ya riadha Afrika

8/4/2018
More
Kenya imekuwa nchi bora katika mashindano ya riadha ya Afrika baada ya kunyakua medali 19, zikiwemo 11 za dhahabu, ikifuatwa na Afrika Kusini na wenyeji Nigeria. Yalikuwa ni mashindano ya 21, yaliyoshuhudia maandalizi mabaya yaliyosababisha mamia ya wanariadha kukwama katika uwanja wa ndege mjini Lagos baada ya kukosa ndege ya kuwapeleka mjini Asaba. Tanzania nayo ilijiondoa. Tunajadili.

Duration:00:23:47

Cecafa na harakati za kuinua soka la wanawake Afrika Mashariki na Kati

7/28/2018
More
Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na harakati za kuinua soka la wanawake baada ya kutamatika kwa michuano ya Cecafa kwa wanawake nchini Rwanda. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samuel John na Aloyce Mchunga kutathimini.

Duration:00:22:40