Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho-logo

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Serikali ya Tanzania yawafunga tembo vifaa maalum

9/9/2018
More
Katika makala haya hii leo tunaangazia hatua ya serikali ya Tanzania kuwafunga Tembo vifaa maalum kwa ajili ya kufuatilia mienendo yao ili kuweza kuwaratibu.

Duration:00:10:24

Fahamu Faida za Biashara Rafiki Wa Mazingira

1/15/2017
More
Hakika msikilizaji wetu utakubaliana naami ya Kwamba Pale popote duniani, uchumi wa wananchi na taifa huimarika kutokana na kushamiri kwa biashara. Iwe inafanywa na sekta binafsi au taasisi.Basi kupitia kipindi cha Mazingira leo,Dunia yako kesho kwa juma hili ingazia juu ya Faida za Biashara Rafiki wa Mazingira katika Utunzaji wa Mazingira yetu katika Nchi zetu za Afrika Mashariki na Kati

Duration:00:10:29

Fahamu Juu ya Umuhimu wa Madili ya Kutunza Mazingira

1/8/2017
More
Maadili ni miongoni mwa vitu muhimu sana katika ujenzi wa jamii yoyote lile, bila uwepo wa nidhamu ya kutosha jamii yoyote ile haiwezi kuendelea. Maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii hauwezi kufikiwa pasipo nidhamu na maadili, Hatuwezi kuwa na jamii yenye mpangilio mzuri pasipo maadili. Basi Makala yetu ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa juma hili inagazi juu ya umuhimu wa Madili ya Mazingira

Duration:00:11:20

Fahamu Juu ya Umuhimu wa Kuhifadhi Misitu

1/1/2017
More
Hakika msikilizaji wetu unakubaliana naami ya kwamba Misitu ni Uhai, kwa kutambua umuhimu wa usemi huu makala yetu inagazia kwa mara nyingine juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu lakini vile vile athari za uharibifu wa Misitu

Duration:00:09:41

Fahamu Mwaka 2016 Kuvunja Rekodi ya kuwa Mwaka wenye Joto Zaidi

11/20/2016
More
Kwa mujibu wa ripoti ya WMO imeainisha hali ya joto kidunia imeongezeka mara dufu mwaka 2015/2016 kutokana na dunia kukumbwa na kipindi cha El Nino, El Nino ni hali ya kuongezeka kwa joto kwenye mstari wa Ikweta katika bahari ya Pacific, kipindi ambacho kinakadiriwa kuwa hujirudia kila baada ya miaka 5, hali hii ilianza kushuhudiwa katikati ya mwaka huu. Zaidi ya hali ya joto kidunia, viashiria vingine vya mabadiliko ya tabia nchi pia vilionesha kufikia kiwango cha juu, limeonya shirika...

Duration:00:10:11

Fahamu juu Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi

11/13/2016
More
Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi umeanza huko Marrakesh, Morocco, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuanza rasmi kutekelezwa kwa mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Ambapo kwenye mkutano huo mada kadhaa zimejadiliwa zikiwamo usaidizi kwa Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uhakika wa chakula na nafasi ya jinsia na vijana Makala ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa Juma hili inagazia juu hali ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na...

Duration:00:10:56

Fahamu juu ya Suala la Ukusanyaji Taka katika Mjii wa Nairobi

10/16/2016
More
Bila Shaka hakuna asiyefahamu kuwa baadhi ya maeneo mengi ya miji yetu ni machafu na uchafu huo huchangiwa sana na mifuko na chupa za plastiki. Kipindi cha Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa juma hili kinangazia juu ya kundi la Vijana la huko Nairobi nchini Kenya ambalo wanaokotoa taka ikiwemo chupa za plastiki,hii ikiwa ni moja ya njia ya kuweka mjii katika hali ya usafi

Duration:00:10:29

Sehemu ya Pili:Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa

10/9/2016
More
Ufugaji wa samaki wa kisasa kwenye mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani kote inchi kama .Niwazi tumeona baadhi ya inchi nyingi zikizidi kuzalisha nafasi nyingi za ajira kwa shughuli hizi pamoja na kukuza kipato cha mhusika mmoja mmoja, jamii flani na taifa kwa ujumla. Katika kuiangalia fursa hii katika sehemu yetu ya pili na ya mwisho ya makala yetu ya Mazingira Leo Dunia Yako Kesho kwa juma hili tutaangalia juu ya mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji...

Duration:00:09:59

Fahamu juu ya Ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia

10/2/2016
More
Ufugaji wa samaki wa kisasakwenye visima au mabwawa ya kuchimbwa umekuwa ukishamiri duniani na Ufugaj huu wa samaki ni sawa kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Katika makala haya ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho kwa juma hili itangazia kwa ujumla kwa juu ya ufugaji wa samaki wa kisasa na mbinu muhimu za kuzingatia wakati wa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki wa kisasa

Duration:00:09:18

Fahamu Athari za magugu maji kwa Mazingira

9/18/2016
More
Suala la kupambana na magugu maji katika ziwa Victoria bado ni changamoto, licha ya kuwepo na jitianda mbali mbali za kupambana na magugu maji katika ziwa hilo. Makala ya Mazinigira Leo,Dunia Kasho ingazia juu ya adhaaa ya Magugu maji katika Ziwa Victoria na athari zake kwa mazingira

Duration:00:10:09

Fahamu Changamoto za Mazingira zinazo likabili Ziwa Victoria

9/11/2016
More
Ziwa Victoria lililopo Kanda ya Ziwa ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya maji na maendeleo ya nchi nyingi katika ukanda wa Afrika Mashariki , nyingine kama vile Tanzania Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na Misri inayopata huduma ya maji ya Mto Nile unaoanzia kwenye ziwa hili la kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la pili kwa ukubwa duniani. Kipindi cha Mazingira leo Dunia Yako kesho kwa juma hili inagazia juu ya changamoto zinazolikabili ziwa Victoria

Duration:00:10:09

Fahamu Faida na Athari za Kimazingira zitokanazo na kuhamisha Mji Mkuu Dodoma kutoka Dar es Salaam

8/28/2016
More
Uamuzi wa serikali ya jamhuri wa Mungano wa Tanzania kuhamia mji mkuu Dodoma kutoka Dar es Salaam imezua mjadala miongoni mwa watalaamu wa Masuala ya Mazingira. Basi wakati ofisi ya Waziri Mkuu ikipanga kuhamia Dodoma mwezi Septemba,Makala yetu ya Mazingira Leo Dunia yako kesho inagazia juu ya Faida na Athari za Kimazingira kwa mjii wa Dodoma

Duration:00:10:18

Fahamu FaidaUfugaji wa nyuki wa kisasa kwa Mazingira

8/21/2016
More
Ufugaji wa nyuki wa kisasa unoazingatia matumizi ya vifaa bora ambao huzalisha asali bora lakini pia husaidia katika utunzaji wa Mazingira lakini pia licha ya kusaidia kutunza mazingira, nyuki ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai vyote, kwani husaidia katika uchavushaji wa mimea. Makala ya Mazingira Leo,Dunia yako Kesho inagazia juu ya faida za Ufugaji wa nyuki wa kisasa katika utunzaji wa Mazingira

Duration:00:10:11

Fahamu Naama ya Kenya Inavyokabiliana na Hali Mabdiliko ya Tabia Nchi

8/14/2016
More
Mabadiliko ya tabia nchi imekuwa miongoni mwa ajenda kuu za Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa Kwa kuona umuhimu wa suala la mabadiliko ya tabia nchi, Serikali ya Kenya Tayari imeanza kuchukuwa hatua za ufuatiliaji, kufanya tathimini na mbinu mbalimbali za kukabiliana na Athari za Mabdiliko ya tabia Nchi, Makala ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho inagazia juu ya hatua serikali ya Kenya inachukuwa katika kukabiliana na hali ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Duration:00:10:26

Fahamu Athari Za Mabadiliko ya Tabia Nchi Kwa Viumbe vya baharini na Matumbawe

8/7/2016
More
Wataalamu mbali mbali wa masuala ya wa sayansi ya baharini wamedai ya kwamba n matumbawe katika mwambao wa bahari ya hindi, haswa kisiwani Zanzibar yapo hatari ya kutoweka kutokana na uharibifu mkubwa wa Mazingira unaotokana na shuhuli za kila siku za binadamu Kipindi chetu cha Mazingira Leo inagazia juu ya tahri za Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa ustawi wa viumbe vya baharini na matumbawe ambayo ndiyo makaazi makubwa ya samaki

Duration:00:10:25

Changamoto ya Utiririshaji wa Maji Taka Mjini na Naama ya Kukabiliana Nayo

7/24/2016
More
Takwaimu za shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa kila sekunde 20 mtoto huafariki kutokana na kipindu pindi au na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu. Basi Makala yetu ya Mazingira Leo Dunia Yako kesho Kwa Juma hili inagazia juu ya jitihada Nchi za Afrika Masharika Na Kati za kutatua tatizo la maji taka na taka ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya kisasa ya kuhifadhi maji taka na kusafisha.

Duration:00:10:57

Fahamu Juu ya Madhimisho ya Wiki ya 6 ya Maji Barani Afrika

7/17/2016
More
Tanzania ni Mwenyeji maadhimisho ya 6 ya wiki ya Maji Barani Afrika na Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika Mkutano huo unakutanisha waadu wa masula ya maji zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbali mbali mbalini afrika huku Kauli mbiu ya mkutano huo mwaka huu ni Kufikia lengo la maendeleo Endelevu Juu ya usalama wa Maji na usafi wa mazingira” Makala ya Mazingira Leo,Dunia Yako Kesho kwa jumaa hiii inajikita kuangazia juu ya Tija la Kongamano hilo la 10 la maji Barani...

Duration:00:11:16

Fahamu Kilimo cha kijani ( Green house) na Faida zake Kwa Mazingira

7/3/2016
More
Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi katika mataifa mengi katika bara la Afrika,hii ni kutokana na sekta hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia pato la taifa haswa kupitia mazao ya Biashara Kupitia Makala yetu juma hili tutangazia juu ya Kilimo cha ndani ya nyumba ya kijani ( Green house) naama Teknolojia hii inavyotumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa

Duration:00:10:20

Fahamu Kilimo Hai

6/19/2016
More
Kilimo hai au organic farming ni aina ya kilimo ambacho huzigatia matumizi endelevu ya rasilimali za mazao ya kilimo pamoja na mifugo. Kilimo hiki hutumia mara nyingi aina ya mbolea isiyotengenezwa viwandani, na ni aina ya kilimo ambacho huzingatia utunzaji wa mazingira. Makala ya Mazingira Leo,Dunia Yako kesho jumaa hili inangazia juu ya Kilimo Hai na faida zake kwa Mazingira

Duration:00:10:40

Umuhimu wa Hifadhi Shirikishi Katika Hifadhi zaTaifa

6/12/2016
More
Uwepo wa hifadhi mbali mbali za taifa pamoja na rasilimali zake katika mataifa yetu katika ukanda huu wa afrika Mashariki na kati,zimekuwa na mchango mkubwa katika mataifa yetu. Hii ni Kutokana na hifadhi hizi, zimekuwa zikichangia kwa kisasi kikubwa katika kukuwa kwa uchumi kutokana na watalii kuzitembelea hifadhi hizo Kutokana na hifadhi hizi kuwa na manufaa makubwa kwa serikali yetu,Serikali ya Tanzania imeazisha Usimamizi Shirikishi wa jamii katika maeneo haya,

Duration:00:09:26