Mjadala wa Wiki-logo

Mjadala wa Wiki

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Hati ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya

12/4/2018
More
Rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya, ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaotakiwa na serikali kwa madai ya kuhusika na mauaji ya rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini humo Melchior Ndadaye mwaka 1993. Tunajadili suala hili kwa kina.

Duration:00:13:16

Marekani: Democratics washinda bunge la wawakilishi, Republican watawala Senate

11/6/2018
More
Chama cha Republican cha rais Donald Trump, kimepata ushindi katika bunge la Senate huku kile cha Denocratic, kikirejesha udhibiti wa bunge la wawakilishi, baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge, Maseneta na Magavana, uliofanyika siku ya Jumanne. Matokeo haya yanamaanisha nini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kujadili hili, ni Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa mjini Arusha nchini Tanzania na Dokta Brian Wanyama, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii mjini Bungoma...

Duration:00:13:13

Rais Paul Biya achaguliwa tena kuongoza Cameroon kwa muhula wa saba

10/23/2018
More
Rais wa Cameroon Paul Biya, ametangazwa mshindi kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa saba, kuendeleza uongozi wake wa miaka 36. Upinzani umekataa kutambua ushindi huu. Ushindi huu una maana gani kwa demokrasia ya Cameroon na bara la Afrika ? Tunajadili.

Duration:00:13:03

Siasa za mashine za kupigia kura nchini DRC

10/9/2018
More
Kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, bado kuna mvutano wa matumizi ya mashine za kupigia kura. Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia yanataka zisitumiwe kwa hofu ya wizi wa kura, lakini Tume ya Uchaguzi CENI, inasisitiza kuwa ni sharti zitumiwe. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili mwafaka kupatikana. Tunajadili hili kwa kina.

Duration:00:14:14

Mjadala wa kura ya maoni nchini Kenya, kuibadilisha Katiba

10/2/2018
More
Mjadala wa kuwepo kwa kura ya maoni nchini Kenya ili kuibadilisha Katiba nchini Kenya, umeanza kupamba moto. Lengo ni kubadilisha mfumo wa uongozi, na kuwepo kwa Waziri Mkuu ili kuleta mshikamano wa taifa kila baada ya Uchaguzi Mkuu.

Duration:00:11:42

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa 73 waanza jijini New York

9/25/2018
More
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa 73, unaendelea jijini New York nchini Marekani. Rais Donald Trump amefungua mkutano huo kwa kuishtumu Mahakama ya Kimataifa ya ICC na kusema haina mamlaka na ni dhaifu. Naye rais wa DRC, Joseph Kabila ameihakikishia dunia kuwa uchaguzi nchini mwake, utafanyika mwezi Desemba kama ilivyopangwa. Tunajadili hili na Dokta Brian Wanyama na Haji Kaburu, wachambuzi wa siasa za Kimataifa.

Duration:00:10:07

Mchakato wa Uchaguzi nchini DRC na kufungwa kwa Bemba

9/18/2018
More
Wiki hii, Mahakama ya Kimataifa ya ICC imemhukumu mwaka mmoja, mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Jean Pierre Bemba, baada ya kupatikana na kosa la kuwahonga mashahidi. Hata hivyo, hatafungwa jela kwa sababu tayari ameshakitumikia kifungo hicho. Je, hii inamaanisha nini kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba ? Tunathathmini na mchambuzi wetu Abdulkarim Atiki.

Duration:00:11:01

Machafuko ya kisiasa na kukamatwa kwa wapinzani Uganda

8/21/2018
More
Tunaangazia kinachotokea nchini Uganda baada ya kukamatwa na kupigwa kwa wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, baada ya machafuko ya kisiasa wiki moja iliyopita mjini Arua, Kaskazini mwa nchi hiyo wakati msafara wa rais Yoweri Museveni ulivyoshambuliwa.

Duration:00:12:08

Mahakama ya Kimataifa ya ICC yatimiza miaka 20

7/17/2018
More
Mahakama ya Uhalifu wa kivita ICC, imetimiza miaka 20 tangu ilipoanza kazi yake katika mjini hague nchini Uholandi. Watu mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kuhusu umuhimu na kazi ya Mahakama hii ya Kimataifa. Je, imefanikiwa kwa muda wa miaka hii Ishirini ? Tunajadili na Wakili na mchambuzi wa siasa za Kimataifa Ojwang Agina akiwa Nairobi nchini Kenya na Omar Kavota Mwenyekiti wa Shirika la kutetea haki za binadamu na kuhimiza uongozi bora CEPADHO, akiwa Mashariki mwa Jamhuri ya...

Duration:00:15:17

Mkataba wa kusitisha vita nchini Sudan Kusini wakiukwa tena

7/3/2018
More
Mkataba wa kusitisha vita kabisa nchini Sudan Kusini, uliotiwa saini na rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, umevunjika. Wamajeshi wanawalaumu waasi, huku waasi wakisema jeshi lilishambulia ngome zao. Nini hatima ya mkataba huu ?

Duration:00:14:53

Mkutano wa kihistoria kati ya rais wa Marekani na Korea Kaskazini

6/12/2018
More
Leo katika Mjadala wa wiki tunajadili, baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano wa kihistoria kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un siku ya Jumanne, nchini Singapore. Mambo mawili makuu yaliyokubaliwa ni Korea Kaskazini kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia lakini pia Marekani ilikubali kusitisha mazoezi ya kijeshi kati ya jeshi lake na lile na Korea Kusini. Nini hatima ya maelewano haya ? Tunajadili.

Duration:00:11:48

Matokeo ya kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba ya Burundi na mustakabali wa taifa hilo

5/22/2018
More
Mjadala wa wiki leo jumatatu ya may 23 tumeangazia kuhusu mustakabali wa taifa la Burundi baada ya kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba, ambayo tume huru ya uchaguzi nchini humo CENI inasema kura ya ndio imeshinda kwa zaidi ya asilimia 70 wakati kura ya hapana ikipata asilimia 19. Kudadavua haya nitakuwa nao Nzeyimana Abdul ambae ni mjumbe wa upinzani unaishi uhamishoni wa CENARED pia Innocent Banno ni mwanasiasa wa upande wa serikali. Upinzani umetupilia mbali matokeo hayo na kuomba...

Duration:00:14:36

Mkutano wa kihistoria kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini

5/1/2018
More
Mwezi Aprili, kulikuwa na mkutano wa kihistoria kati ya viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskzini baada ya muda mrefu wa vita baridi kati nchi hizi jirani. Mkutano kati ya Jim Jong Un kiongozi wa Korea Kaskazini na Moon Jae-in rais wa Korea Kusini ulifanyika mpakani mwa nchi hizo mbili na kufikia makubaliano ya kuanza upya ushirikiano kati ya Pyongyanga na Seoul. Kukutana na viongozi hawa kulikuwa na umuhimu gani na kunaamaanisha nini ?

Duration:00:13:35

Marais wa Afrika kutia saini mkataba wa soko la pamoja

3/20/2018
More
Wakuu wa nchi za Afrika, wamekutana jijini Kigali nchini Rwanda kutia saini mkataba wa kuwezesha biashara huru na soko la pamoja.Je, hatua hii inamaanisha nini ? Tunajadili.

Duration:00:11:40

Kwanini rais wa Uganda Yoweri Museveni alimfuta kazi Inspekta wa Polisi ?

3/6/2018
More
Wiki hii, rais wa Uganda Yoweri Museveni, alimfuta kazi Waziri wa usalama Henry Tumukunde na Inspekta Mkuu wa Polisi Jenerali Kale Kayihura. Uamuzi huu wa rais Museveni haukutarajiwa. Kujadili hili tunaugana na Dokta Kizza Besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda ambaye amekuwa akiwania urais tangu mwaka 2001, lakini pia Kenneth Lukwago mchambuzi wa siasa za Uganda.

Duration:00:13:42

Nini hatima ya rais Jacob Zuma ?

2/6/2018
More
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anaendelea kukabiliwa na shinikizo za kujiuzulu kwa madai ya ufisadi. Zuma ambaye amekuwa rais tangu mwaka 2009, amekataa kujiuzulu.Hotuba yake iliyokuwa imepangwa kufanyika siku ya Alhamisi, imeahirishwa. Nini hatima ya rais Zuma ? T

Duration:00:13:12

Hatima ya maandamano dhidi ya rais Kabila nchini DRC

1/23/2018
More
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema litaendelea kupanaga maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila kuondoka madarakani, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.Umoja wa Mataifa, unasema watu sita walipoteza maisha wakati wa maandamano Jumapili iliyopita. Tunajadili hatima ya maandamano haya.

Duration:00:11:36

Palestina yasema haitaitambua Israel

1/16/2018
More
Mamlaka ya Palestina imesema, haitaitambua Israel baada ya Marekani kutangaza kuwa inaitambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel. Wakati uo huo, Marekani imesema inasitisha msaada wa fedha kwa Tume ya Umoja wa Mataifa, inayowashughulikia wakimbizi wa Kipalestina.

Duration:00:15:01

Upinzani walalamikia kusumbuliwa Burundi

1/9/2018
More
Serikali ya Burundi, inaendelea na mchakato wa kuibadilisha Katiba ili kuruhusu mgombea urais kuongoza kwa muda wa miaka saba badala ya mitano. Upinzani unalalamika kuwa, wanasiasa na wanaharakati wake wanakamatwa na kuzuiwa wanapojaribu kuwashawishi wananchi kukataa mchakato huo. Tunachambua hili.

Duration:00:15:52

Mjadala Kuhusu Sintofahamu ya Kisiasa nchini DRC na Ushiriki wa Kanisa Katoliki

1/2/2018
More
Makala ya Mjadala wa Wiki Juma Hili Inazungumzia Sintofahamu ya Kisiasa Nchini DRC Ambapo Juma Moja Lililopita Kanisa Katoliki Liliitisha Maandamano Ambayo Hata Hivyo Yalikabiliwa Vilivyo na Vyombo Vya Dola ambapo Watu Kadhaa Walipoteza Maisha Kwenye Maandamano Haya. Wanasiasa Kutoka chama Tawala na Wale wa Upinzani Wameshiriki Kwenye Mjadala Huu.

Duration:00:13:29