Mtazamao Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii-logo

Mtazamao Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Wapinzani wawili DRC waondoa saini zao kuunga mgombea mmoja, Waganda watakiwa kulinda wachina, moto waua watu California

11/16/2018
More
Makala ya wiki hii imeangazia hatua ya wanasiasa wawili wa upinzani: Felix Tshisekedi wa UDPS na Vital Kamerhe kiongozi wa chama cha UNC kuondoa saini zao kuhusu uteuzi wa mgombea Martin Fayulu kupeperusha bendera ya upinzani, katika uchaguzi wa desemba 23 mwaka huu.Nchini Tanzania serikali ilisema itanunua korosho zote nchini, kimataifa tumeangazia Uingereza na Brexit mpango wa kujiondoa umoja wa ulaya

Duration:00:20:21

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo achaguliwa katibu mkuu mpya wa Francophonie, Upinzani DRC wazuwiwa kukutana Lubumbashi

10/12/2018
More
Mkutano wa Viongozi wa jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa Francophonie, OIF umetamatika juma hili huko Erevan nchini Armenia, ambapo viongozi hao wamemteuwa waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo, kuchukuwa nafasi ya Michaelle Jean. Huko DRC joto la kisiasa laendelea kupanda, wakati kimataifa Uturuki na Marekani zachunguza kupotea kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi

Duration:00:21:26

Kuzama kwa kivuko Ziwani Victoria nchini Tanzania

9/21/2018
More
Tanzania inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 200 waliozama katika Ziwa Victoria, kurejea kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi nchini Uganda na Tume ya Uchaguzi nchini DRC, kutangaza majina ya wagombea urais mwezi Desemba.

Duration:00:19:26

Polisi wa Uganda wakabiliana na waandamanaji kaskazini mwa nchi hiyo, hati ya kimataifa ya kukamatwa Katumbi yatolewa

8/17/2018
More
Makala hii imeangazia hatua ya kufikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa mbunge wa Uganda na mwanamuziki nguli Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine, kwa madai ya kumiliki silaha kinyume cha sheria baada ya kukamatwa kwake, lakini pia waziri wa sheria nchini DRC kutoa waranti wa kimataifa kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi, na kimataifa kifo cha mwanamziki wa mtindo wa soul huko Marekani, Aretha Louise Franklin.

Duration:00:21:18

Rais Joseph Kabila wa DRC asema hatowania urais, Tanzania na Kenya zaadhimisha miaka 20 ya shambulio la kigaidi

8/10/2018
More
Katika makala hii tumeangazia hatua ya rais wa DRC Joseph Kabila kutangazawaziri wa zamani wa mambo ya ndani,Emmanuel Ramazani Shadary, kupeperusha bendera ya chama tawala cha PPRD katika uchaguzi wa urais wa desemba 23, pia Tanzania na Kenya juma hili ziliadhimisha miaka ishirini ya mashambulizi ya balozi za Marekani jijini Daresalaam na Nairobi, wakati uchaguzi wa Zimbabwe wampa ushindi Emmerson Mnangagwa, na kimataifa hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kuiwekea vikwazo Iran....

Duration:00:21:04

Chama cha MLC chamuidhinisha JP Bemba kuwa mgombea, Burundi yakanusha shutuma za Rwanda, wafaransa waadhimisha siku ya uhuru

7/13/2018
More
Makala hii imeangazia kuhusu vyama vya Upinzani nchini DRC kupinga matumizi ya mashine za kielektroniki, wakati chama cha MLC chamtangaza JP-Bemba kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa desemba 23, Jeshi la Burundi lilitupilia mbali tuhuma kuwa kuna watu wenye silaha waliovuka mpaka na kuingia nchini Rwanda kufanya mashambulizi na kisha kurudi nchini Burundi, Serikali ya Uganda kuangalia upya kodi ya mitandao ya kijamii, na leo Wafaransa waadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi ya...

Duration:00:21:04

Kesi dhidi ya Katumbi kuahirishwa hadi mwezi Oktoba, watu 15 wauawa katika ajali ya moto jijini Nairobi Kenya

6/29/2018
More
Katika makala hii mtangazaji ameangazia hatua ya mahakama kuu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya kuahirisha hadi oktoba 10, kesi ya mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi kwa madai kuwa aliwaajiri mamluki kutoka Marekani, siasa za Burundi, watu 15 kupoteza maisha katika ajali ya moto katika soko la Gikomba, jijini Nairobi.Pia kimataifa maandalizi ya mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Vladmir Putin lakini pia viongozi wa ulaya kuafikiana kuhusu wahamiaji.

Duration:00:21:01

Ziara ya rais Paul Kagame nchini Ufaransa, Mabango yenye picha ya rais Kabila yaonekana jijini Kinshasa

5/25/2018
More
Wiki hii miongoni mwa habari zetu kuu zilizopewa uzito katika matangazo yetu ni pamoja na ziara ya rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Ufaransa, ambapo waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo bi Louise Mushikiwabo amegombea kiti cha ukatibu mkuu wa jumuia ya nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa, mabango yenye picha ya rais Joseph Kabila kuonekana Kinshasa, kimataifa tumeangazia mkutano wa rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa korea Kaskazini.

Duration:00:21:09

Marekani yahamishia ubalozi wake Jerusalem, rais wa DRC Joseph Kabila kuwania muhula wa tatu, kura ya maoni Burundi

5/18/2018
More
Makala hii imeangazia kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi mjini Jerusalem, chama tawala cha nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo cha PPRD kumpendekeza rais Joseph Kabila anayemaliza muda wake kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu, wakati kimataifa kauli ya rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa maandalizi ya mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yako palepale.

Duration:00:21:06

Kampeni ya kura ya maoni yaanza nchini Burundi, Ziara ya mkuu wa ICC Fatou Bensouda DRC, na uchaguzi wa nchini Armenia

5/4/2018
More
Katika makala hii imeangaziwa hatua ya serikali ya Burundi ya kupiga marufuku matangazo ya vyombo vya kimataifa BBC na VOA kwa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 07 mwezi mei, ziara ya mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na hali kadhalika hotuba ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mbele ya baraza la Senate pamoja na wabunge nchini humo, wakati kimataifa uchaguzi wa nchini Armenia, pamoja na mambo mengine

Duration:00:21:03

Chama cha UDPS na mkutano wake mkubwa Kinshasa, Rais Kenyatta wa Kenya aeleza siasa nchini mwake, Mkutano wa viongozi wa Korea

4/27/2018
More
Makala ya wiki hii imeangazia hatua ya viongozi wa serikali ya Kinshasa kuruhusu mkutano wa chama cha UDPS kinachoongozwa na Felix Tshisekedi, wakati huko Kenya rais Kenyatta amesema mkutano wake na kiongozi wa upinzani haukuwakufurahisha watu wengi nchini humo, tumegusia siasa za ukanda wa afrika mashariki na kati wakati kimataifa dunia imeshangazwa na mkutano wa viongozi wa Korea zote mbili.

Duration:00:21:04

DRC: tume ya uchaguzi kudhibiti watu waliojiandikisha mara mbili, makamisheni wa IEBC nchini Kenya wajiuzulu, Trump kukutana na Kim Jon Un

4/20/2018
More
Makala hii imeangazia hatua ya tume ya uchaguzi nchini jamhuri ya kidemokrasia ya CENI, kuanza kuwashughulikia watu ambao walijiandikisha mara mbili kama wapiga kura,na kuwapeleka mahakamani, lakini pia tamko wa wabunge wa Kivu Kaskazini wakipinga kauli ya rais kabila akiwatuhumu watu wa Jamii wa wanande kule Mashariki mwa DRC, kujiuzulu kwa makamisheni watatu wa tume ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC wakati kimataifa tumengazia mpango wa rais Trump kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim...

Duration:00:21:09

Mkutano wa wafadhili kuhusu DRC wafanyika Uswis, mazishi ya Winnie Mandela pia Marekani na suala la Syria

4/13/2018
More
Katika makala hii umeangaziwa mkutano wa wafadhili kuchangisha pesa kwa ajili ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kuhusu hali ya kibinadamu nchini humo wafanyika mjini Geneva uswis, lakini pia mazishi ya mama mwanaharakati aliyepinga utawala wa kibaguzi nchini Afrika kusini, bi Winnie Mandela yafanyika mjini Soweto, pamoja na yaliyojiri Rwanda, Kenya, Tanzania na kwingineko dunia, makala hii imegusia mvutano kati ya mataifa ya magharibi na Urusi kuhusu Syria.

Duration:00:21:25

Kifo cha Winnie Mandela aliyekuwa mke wa Nelson Mandela, DRC yakataa kushiriki mkutano wa Geneva, Syria hali si shwari

4/6/2018
More
Katika makala ya juma hili tumeangazia kifo cha Winnie Mandela ambaye alikuwa mke wa rais wa kwanza mweuzi nchini Afrika kusini, hali ya usalama yaendelea kuzorota mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo huku serikali ya nchi ikiendelea na msimamo wake wa kutoshiriki katika mkutano wa Geneva kuhusu haki za binadamu, na mgomo wa wafanyakazi wa reli nchini Ufaransa, na mambo mengine

Duration:00:21:06

Tume ya umoja wa mataifa DRC yaongezewa muda wa mwaka mmoja, Kiongozi wa Korea kaskazini azuru China

3/30/2018
More
Katika makala hii tumeangazia hatua ya baraza la usalama la umoja wa mataifa ya kuiongezea Monusco mwaka mmoja zaidi lengo likiwa ni kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu desemba 23 mwaka huu, lakini pia wakimbizi 1600 wa Burundi waliokuwa Rwanda warejeshwa nyumbani, na kimataifa ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini nchini China. Karibu kujiunga na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka, kusikiliza zaidi

Duration:00:20:38

Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga akutana na rais Uhuru Kenyatta, mauaji mapya DRC

3/9/2018
More
Makala hii imeangazia hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kukutana na rais Uhuru Kenyatta mwishoni mwa juma, mauaji ya watu sita katika maeneo ya Eringeti wilayani Beni mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, serikali ya Rwanda yaanza kufunga makanisha, wakati kimataifa rais Trump wa Marekani kukubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwezi mei mwaka huu.

Duration:00:21:25

Maandamano ya kanisa katoliki na wanasiasa wa DRC, upinzani wa Burundi wapinga michango ya Uchaguzi

1/19/2018
More
Katika makala hii tumeangazia kuhusu mgawanyiko ulioshuhudiwa kati ya wanasiasa wa rassemblement wa upande wa waziri mkuu Bruno Tshibala nchini DRC kuhusu maandamano ya jumapili ya january 21, nchini Burundi wapinzani wapinga michango ya wananchi kuhusu uchaguzi nchini humo, Rwanda na Tanzania,zakubaliana kuhusu ujenzi wa reli kati ya mataifa hayo mawili, wakati kimataifa tumeangazia ziara ya rais wa Ufaransa nchini Uingereza, lakini pia siasa za Syria.

Duration:00:21:11

Mvutano kati ya kanisa katoliki na serikali ya DRC waendelea, upinzani nchini Uganda kupinga marekebisho ya katiba

1/12/2018
More
Katika makala hii tumeangazia mvutano unaoendelea kushuhudiwa kati ya kanisa katoliki na serikali ya DRCongo tangu polisi kuvamia na kurusha mabomu ya kutoa machozi makanisani mjini Kinshasa juma moja lililopita; mpango wa upinzani wa Uganda kupinga marekebisho ya kipengele kinachohusu umri wa mtu anayetaka kuwania urais, siasa za Kenya, Zimbabwe, na kimataifa kauli ya rais wa Marekani kuhusu Afrika na Haiti, ambayo imezua mijadala kote duniani.

Duration:00:21:07

Wanajeshi wa Umoja wa mataifa kutoka Tanzania wauawa Beni DRC, mvutano wa ndani ya chama cha UDPS, DRC

12/15/2017
More
Katika makala hii tumeangazia mauaji ya wanajeshi kumi na wanne wa umoja wa mataifa kutoka Tanzania mjini Beni, mashariki mwa Congo, waziri mkuu wa DRC Bruno Tshibala amesema yeye ndiye kiongozi wa chama cha upinzani cha UDPS, mkutano wa viongozi wa nchi5 za Sahel pamoja na suala la Uingereza kujivua uanachama wake katika umoja wa ulaya, ni miongoni mwa mambo mengine. Karibu kusikiliza makala hii na mwandishi Reuben Lukumbuka

Duration:00:21:34

Wanajeshi wa kulinda amani wauawa nchini DRC

12/8/2017
More
Kuuawa kwa wanajeshi wa kulinda amani raia wa Tanzania 14 nchini DRC, kutopatikana kwa mkataba katika mazungumzo ya kisiasa ya Burundi na hatua ya Marekani kutambua mji wa Jerusalem kuwa maka makuu ya Israel ni miongoni mwa masuala makubwa yaliyojiri wiki hii.

Duration:00:19:21