Nyumba ya Sanaa-logo

Nyumba ya Sanaa

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Khadija Kopa;Nakubalika zaidi nikiimba Taarab za Mipasho

9/14/2018
More
Muziki wa Taarabu ulianza kushamiri Miaka ya 1990 nchini Tanzania na Miongoni mwa Waanzilishi wa Bendi ya Tanzania One Theatre TOT ni Khadija Omari Kopa. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Khadija Omary Kopa katika sehemu ya kwanza ya makala hayo.

Duration:00:20:04

Mbanaye Bendi ya Malawi wamepania Kuutangaza Muziki wa Asili

8/31/2018
More
Walianza kikiwa ni kikundi cha vijana wanane baadae ikawa bendi kamili na kusheheni muziki wa Makabila mbalimbali kutoka nchini Malawi. Katika Makala ya Nyumba ya sanaa, Steven Mumbi anazungumza na mmoja wa wasanii wa Bendi hiyo Gilbert Simchoba kuzungumzia safari ya Benki hiyo yenye miaka minne sasa.

Duration:00:20:49

Nyahoga;Ubunifu wa Mavazi umenifanya niheshimike

8/24/2018
More
Mbunifu wa Mavazi Agnes Nyahoga anajivunia kuwa Mbunifu baada ya kufanya kazi ya kuuza chakula bila mafanikio na kuamua kufanya kazi Hotelini,akashawishika kujifunza ubunifu . Ungana na Mtayarishaji wa Makala ya Nyumba ya Sanaa Steven Mumbi kuhusu safari yake ya Ubunifu,na namna alivyofanikiwa kuifikia ndoto yake.

Duration:00:20:28

SIGE LUCAS;Uchoraji unaakisi Maisha ya Waafrika

8/3/2018
More
Sanaa ya Uchoraji picha si tu imekuwa sehemu ya ajira kwa vijana nchini Tanzania bali imekuwa sehemu ya maisha na ndoto ya watoto kuja kuwa wachoraji wakubwa,kwa kufanya kazi wanazozipenda Maishani. Ungana na Steven Mumbi akiongea na Mchoraji na Mwalimu wa sanaa hiyo Sige Lucas katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa

Duration:00:19:59

Abdul Kingo;Uchoraji wa Vibonzo umebadili Maisha ya Watawala.

7/13/2018
More
Uchoraji wa Vibonzo umekua na umuhimu katika kufikisha ujumbe kwa njia ya Mchoro unaowaelezea wahusika kwa njia ya Mafumbo. Steven Mumbi amezungumza na Mchoraji wa Vibonzo Abdul Kingo, katika Makala ya Nyumba ya Sanaa kuangazia umuhimu wa Sanaa hiyo na Faida yake kwa jamii.

Duration:00:18:40

Mwigune;Muziki wa Jukwaani Unalipa,Vijana tujikite

7/7/2018
More
Tulizo Bendi inaundwa na vijana wa Kitanzania waliojitoa kufanya Muziki wa majukwaani,na kubadili mtizamo wa kuwa muziki ni uhuni na sasa kuwa sehemu ya maisha kwa kujikimu. Steven Mumbi anazungumza na James Mwigune Kiongozi wa Bendi hiyo inayofanya shughuli za kimuziki nchini Tanzania

Duration:00:20:18

Mariagoreth:Ushairi una nafasi ya kuleta Mabadiliko

6/15/2018
More
Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake. Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha...

Duration:00:20:13

Natty OJ ;Muziki wa Reggae umewezesha kuleta amani kwa Vijana nchini Kenya

6/1/2018
More
Msanii wa Muziki wa Reggae kutoka Mombasa nchini Kenya Natty OJ anasema Muziki wake umefanikiwa kubadili mitizamo potofu ya vijana kuhusu Siasa,Uchumi na Maisha kwa Ujumla. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Natty OJ Katika Makala haya.

Duration:00:20:07

Nsamila; Upigaji Picha ni fursa ya ajira kwa Vijana wa Kitanzania

5/4/2018
More
Hapo awali Upigaji picha ilikuwa ni jambo la kujifurahisha na kutunza kumbukumbu za matukio ya kifamilia pekee na ilikuwa nadra sana,vijana kuwa na ndoto za kuwa wapiga picha hii leo imekuwa sehemu ya ajira kwa vijana wengi. Kutana na Imani Suleiman Nsamila kijana wa kitanzania aliye jiajiri kupiga picha akizungumza na Steven Mumbi kuhusu safari yake ya upigaji picha.

Duration:00:20:17

Natasha;Utunzi wa Filamu Umepiga hatua kubwa nchini Tanzania

4/6/2018
More
Uigizaji nchini Tanzania umekuwa na Historia ndefu na Waigizaji wamepitia vipindi tofauti tofauti licha ya changamoto zilizopo lakini bado filamu za kiswahili zimeendelea kustawi. Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumzia sanaa ya uigizaji wa Filamu za Kiswahili.

Duration:00:20:27

Sanaa ya Muziki wa injili na Sheila Glory

12/8/2017
More
Katika makala haya utasikia kuhusu safari ya muimbaji wa muziki wa injili Sheilah Glory kutoka Kenya , alipotoka,alipo sasa na matarajio yake ya siku za usoni. Karibu

Duration:00:21:56

FIlamu na vichekesho Tanzania

10/27/2017
More
Katika makala haya msikilizaji utasikia mengi kuhusu sanaa ya filamu na vichekesho kutoka kwa wasanii wa Timamu African Media ya Dar es Salaam Tanzania kama Ebitoke, Bwana Mjeshi na Mr. Beneficial , karibu

Duration:00:22:20

Sanaa ya filamu Tanzania

10/13/2017
More
Leo katika makala haya utasikia mengi kuhusu sanaa ya filamu nchini Tanzania na Cloud 112 aliyetembelea studio za rfikiswahili Dar es Salaam Tanzania

Duration:00:22:15

Sanaa ya Ubunifu wa mavazi

9/29/2017
More
Katika makala haya utasikia mengi kuhusu sanaa ya ubunifu wa mavazi kutoka kwa mbunifu wa Tanzania Manju Msita, Karibu

Duration:00:18:27

Dazla Msanii wa kizazi kipya na ndoto za kuiwakilisha Pwani ya kenya kimataifa

9/8/2017
More
Kutana na msanii Dazla mwenyeji wa Mombasa Pwani ya Kenya ambaye amepania kuiwakilisha kaunti yake kimataifa kupitia muziki wa kizazi kipya.

Duration:00:20:15

Jamii na sanaa

8/18/2017
More
Katika makala haya utamskia msanii Hamis Magesa Ramadhan au Mac Fish akizungumzia suala la uzalendo katika wimbo wake mpya uitwao Mzalendo, ambao unampongeza pia rais wa Tanznaia kwa moyo wa uzalendo kwa taifa hilo. karibu.

Duration:00:20:39

Sam Luhende;mtayarisha muziki anayejivunia kuwang'arisha wasanii wakubwa wa muziki Tanzania

8/11/2017
More
Sanaa ya utengenezaji na utayarishaji wa muziki si ngeni masikioni mwa waliowengi,leo makala ya nyumba ya sanaa imemtembelea mtayarishaji wa muziki jijini Dar es salaam Sam Luhende,ambaye kazi zake ziliwang'arisha waimbaji kadhaa na kujulikana nje ya mipaka ya Tanzania...

Duration:00:21:16

Sanaa inavyotumiwa kuhimiza amani nchini Kenya

7/21/2017
More
Kenya na Rwanda, zinajiandaa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka 2017. Mwanamuziki wa Kenya Natty OJ mwenye makaazi yake mjini Mombasa, amezindua wimbo maalum wa kuhimiza amani nchini humo kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu. Amezungumza na Martha Saranga.

Duration:00:21:24

Muziki wa kizazi kipya

6/30/2017
More
Katika makala haya kutana na Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Salim Mangija na ufahamu mengi kuhusu yeye na kazi zake za sanaa ya muziki wa kizazi kipya, karibu.

Duration:00:21:35

Lidya Paul Msanii chipukizi katika muziki wa injili na ndoto ya kuigusa jamii

6/23/2017
More
Kutana na msanii anayechipukia katika sanaa ya muziki wa Injili nchini Tanzania Lidya Paul.Ametembelea Rfikiswahili kuzungumzia sanaa yake akijiandaa kuzindua album ya kwanza aliyoita Asante.Karibu

Duration:00:20:52