Nyumba ya Sanaa-logo

Nyumba ya Sanaa

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Nyumba ya Sanaa - Ngumba; Uchoraji wa Picha Halisi unavutia Watalii

10/14/2019
More
Sanaa ya Uchoraji wa picha Halisi ni Sanaa nyingine inayopendwa nchini Tanzania, kutana na Mchoraji Agasto Ngumba akizungumzia Sanaa hiyo katiak Makala haya.

Duration:00:20:02

Nyumba ya Sanaa - Wadatoga na Wamasai wanajivunia Sanaa ya Uimbaji nchini Tanzania

10/14/2019
More
Wadatooga (pia huitwa Wataturu au Wamang'ati) ni kabila la watu wa Kiniloti nchini Tanzania wanaoishi hasa katika mikoa ya Manyara, Mara, Arusha na Singida. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na kikundi cha WADACA kutoka Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania.

Duration:00:20:01

Nyumba ya Sanaa - Kutana na Mchoraji wa Vibonzo 'Muhidin Msamba'

8/26/2019
More
Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Mchoraji wa Vibonzo Muhidini Msamba kuhusu safari yake ya sanaa na Mapokeo ya sanaa hiyo kwa Ujumla.

Duration:00:20:05

Nyumba ya Sanaa - Malkia Queens; Wasichana Wasanii wanaojivunia kuwa Wachoraji

6/11/2019
More
Upatikanaji wa Vifaa,Gharama pamoja na Uelewa Duni vinachangia Sanaa ya Uchoraji kushindwa kusonga Mbele. Malkia Queens wazungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.

Duration:00:20:07

Nyumba ya Sanaa - Monalisa;Kazi za Sanaa za Wanawake hazijanadiwa vya kutosha

6/11/2019
More
Makala ya Nyumba ya Sanaa inaangazia changamoto wanazokabiliana nazo wanawake Waigizaji kiasi cha kuwalazimisha kugeukia kazi nyingine ili kujipatia kipato. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Wasanii mbalimbali nchini Tanzania.

Duration:00:20:05

Nyumba ya Sanaa - Wawanawake waaswa kujitokeza kufanya Sanaa za Mikono

6/11/2019
More
Nyumba ya Sanaa inaangazia Sanaa ya Ususi ama Ufumaji kutoka Mkoani Morogoro Nchini Tanzania. Mtangazaji wa Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Kiongozi wa Kikundi cha Mkonge Sisal.

Duration:00:19:57

Nyumba ya Sanaa - Hali ya Muziki na Wanamuziki wa Tanzania

5/16/2019
More
Kutana na Imelda Munyaga Mwalimu wa Sanaa za aina mbalimbali. Katika Makala haya anazungumza na Steven Mumbi kuhusu Sanaa ya Muziki na Uigizaji.

Duration:00:19:57

Nyumba ya Sanaa - 'Waimbaji wa Muziki wa Injili Wabadilike'

4/29/2019
More
Allain Nyangasa awataka Waimbaji wa Muziki wa Injili kubadilika kufanya Muziki wa Injili kwa ajili ya kumtumikia Mungu na si Biashara Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Msanii huyo.

Duration:00:20:00

Nyumba ya Sanaa - Mloka;Ushairi wa zamani ulikuwa unakonga nyoyo za Wengi

4/9/2019
More
Ushairi ni Sanaa iliyotumika kukuza Lugha ya Kiswahili katika Nchi za Afrika Mashariki,ikiwemo Tanzania hasa wakati wa kupigania uhuru na hata baada ya Uhuru katika kuhamasisha watu kufanya Maendeleo. Steven Mumbi amezungumza na Mshairi wa siku nyingi nchini Tanzania,Charles Mloka, Ungana nae katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.

Duration:00:19:58

Nyumba ya Sanaa - S.Kide;Muziki wa Singeli Utafika mbali kama wawekezaji watajitokeza

4/9/2019
More
Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaochipukia nchini Tanzania,vijana wanajaribu kuifikia hadhira kwa kutumia maudhui ya Asili. Katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa,Ungana na Steven Mumbi akizungumzia Muziki huo akiwa na S.Kide pamoja na Kiongozi wa Wakupeti Band.

Duration:00:20:01

Nyumba ya Sanaa - Maida;Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi imeniwezesha kuwa Mbunifu wa Majengo

3/26/2019
More
Maida waziri Mwanamke aliyeamua kufanya kazi ya Sanaa na hatimaye kufanikiwa kuwa Mbunifu wa Majengo. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Maidfa Waziri kuhusu safari yake katika Sanaa ya Ubunifu

Duration:00:19:59

Nyumba ya Sanaa - Usambazaji wa Filamu wawa kikwazo cha Sanaa ya Uigizaji Kuendelea Tanzania

3/19/2019
More
Filamu za Kiswahili ni Miongoni mwa Filamu zinazopendwa sana katika nchi za Afrika Mashariki si kutokana na kuwa zinatumia lugha adhimu ya Kiswahili tu bali pia ni kutokana na Maudhui na upekee zilionao. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia Sanaa hii na changamoto zinazowakabili Waigizaji nchini Tanzania

Duration:00:20:00

Nyumba ya Sanaa - Cocodo; Vijana tujitume zaidi kwenye Muziki

3/11/2019
More
Hii ni Sehemu ya Pili ya Makala haya tukiangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini Tanzania Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii Remi na Nelius wakizungumzia safari yao ya kimuziki kwa zaidi ya miaka nane sasa

Duration:00:20:02

Nyumba ya Sanaa - Cocodo; Vijana Hawajawekeza kufanya Muziki wa Asili kikamilifu

3/11/2019
More
Katika Makala haya Tunaangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini Tanzania Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Lemi na Nelius wakizungumzia Safari yao ya kimuziki katika Sehemu hii ya kwanza.

Duration:00:20:01

Nyumba ya Sanaa - Mubanga; Watunzi wa Vitabu Wafuate hatua za Utunzi

2/26/2019
More
Teknolojia ina athari gani katika Utunzi wa Vitabu? Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Clement Mubanga Mtunzi wa vitabu katika Makala ya Nyumba ya sanaa.

Duration:00:19:59

Nyumba ya Sanaa - Kimbokota; Sanaa ya Ubunifu haijawekezwa ipasavyo Mashuleni

2/18/2019
More
Sanaa ya Ubinufu ndio sanaa mama katika Uchoraji,Uchongaji na hata katika matumizi ya vyuma chakavu katika kuunda Vifaa mbalimbali. Katika Makala ya Nyumba ya Sanaa Ungana na Steven Mumbi akizungumzuza na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Safina Kimbokota wakizungumza Sanaa hiyo na Mapokeo ya wanafunzi kusoma Sanaa katika elimu ya juu.

Duration:00:19:55

Nyumba ya Sanaa - Sisi Tambala Band wataka Vijana kujikita katika Muziki wa Asili

2/13/2019
More
Sisi Tambala Bendi ni Bendi ya Muziki wa Asili kutoka Tanzania, iliundwa mwaka 1997, tayari imefanya maonesho ya jukwaani katika Nchi Mbalimbali Duniani ikiwa ni pamoja na nchi za Ulaya, Asia na Afrika. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kiongozi wa Bendi hiyo Nanjuja Nanjuja pamoja na wasanii wanaounda bendi hiyo katika Makala ya Nyumba ya Sanaa wakizungumzia Mfanikio yao kimuziki.

Duration:00:20:30

Nyumba ya Sanaa - Siku ya Upigaji Picha Duniani yaadhimishwa Tanzania

2/6/2019
More
Kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya upigaji picha za Habari, Picha zinazoelezea hali wanazokabiliana nazo wananchi katika mataifa Mbalimbali, kutoka barani Afrika ni asilimia 2 tu ya picha hizo huonekana Duniani. Katika Makala ya Nyumba ya Sanaa Steven Mumbi anaangazia umuhimu wa Upigaji Picha za Habari.

Duration:00:20:00

Nyumba ya Sanaa - Belamy;Natarajia kushirikiana na Diamond katika Nyimbo zangu siku zijazo

2/6/2019
More
Sanaa ya Muziki inaendelea kukua kila kukicha nchini DRC, Katika Mji wa Goma sanaa hii inasonga mbele licha ya changamoto zilizopo, anatarajia kushirikiana na wasanii wa nchi za Kenya na Tanzania katika nyimbo zake. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Belamy Paluku katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.

Duration:00:20:01

Nyumba ya Sanaa - Muziki wa Reggae utafika mbali kama Wasanii wataamka

2/6/2019
More
Sixmond Mdeka Maarufu Ras Six alianza na kibao Sina Pamba kilifanya vizuri mwanzoni mwa miaka ya 2000 sasa amedhamiria kuufanya muziki wa Regae katika sura ya kisasa kuwafikia vijana zaidi kupitia Bendi yake. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ras Six.

Duration:00:19:54