Siha Njema-logo

Siha Njema

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Fistula inatibika jamii yatakiwa kuwasaidia waathirika

6/25/2018
More
Jamii imetakiwa kuwasaidia waathirika wa fistula badala ya kuwabagua na kuwanyanyasa.Tatizo la Fistula linatibika kwa nchini Tanzania matibabu hutolewa bure katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam..fuatilia zaidi makala haya.

Duration:00:08:56

Fahamu tatizo la Autism au usonji na namna ya kukabiliana nalo

6/14/2018
More
Makala ya siha njema juma hili inaangazia usonji,kitaalamu Autism ambapo shuhuda Lucy Ruhasha mtanzania anasimulia namna alivyogundua tatizo hilo kwa mwanae wa kwanza na kukabiliana nalo...

Duration:00:09:48

Jema Baruani,Mtanzania anayeshuhudia kupona saratani ya mitoki

4/23/2018
More
Makala ya siha njema inaangazia saratani ya mitoki baada ya kutembelewa na shuhuda aliyeugua na kutibiwa ugonjwa huo nchini Tanzania Jema Baruani ambaye anatoa hamasa kwa jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua hali ya afya kabla ya kushambuliwa na magonjwa.Karibu

Duration:00:10:17

Kifafa cha mimba kinachangia vifo vya wajawazito na watoto

10/30/2017
More
Wataalamu wanaangazia vifo vya watoto wachanga na wajawazito vinacvyochangiwa na tatizo la kifafa cha mimba katika siku za hivi karibuni.Daktari Daniel Nkungu bingwa wa matatizo ya kina mama akiwa Dar es salaam anazungumzia tatizo hili....

Duration:00:10:05

Uganda yathibitisha virusi vya Murbag

10/23/2017
More
Karibu katika makala ya Siha Njema leo tunaangazia virusi vya Murbag ambavyo vimethibitika kuwepo nchini Uganda.Watu wawili wameelezwa kufariki dunia wakati huu kadhaa wakitengwa na kufanyiwa uchunguzi wa kiafya..kujua zaidi fuatana nami ..

Duration:00:09:17

Ugonjwa wa saratani ya matiti unatibika

10/16/2017
More
Katika makala ya Siha njema,wakati dunia inapohimiza uelewa kwa jamii kuhusu ugonjwa wa saratani mnamo mwezi oktoba.Jamii inapaswa kufahamu kuwa ugonjwa huu unatibika..

Duration:00:10:10

Afya ya akili mahali pa kazi

10/9/2017
More
Umoja wa mataifa unaadhimisha siku ya afya ya akili chini ya kauli mbiu afya ya akili mahali pa kazi.Nini wajibu wa muajiri na muajiriwa kuhakikisha tatizo la afya ya akili haliwapati kazini?

Duration:00:09:44

Ugonjwa wa kipindupindu watishia afya za wakazi Mashariki mwa DRCongo

10/2/2017
More
Makala ya Siha njema inaangazia ugonjwa wa kipindupindu uliopiga nchini DRC hivi karibuni na kuathiri idadi kubwa ya wakazi.Waziri wa afya jimboni kivu kaskazini na daktari mtafiti wanaangazia namna jami hiyo inavyokabiliana na maradhi hayo.

Duration:00:10:39

Lishe duni yachangia ongezeko la vifo katika jamii

9/18/2017
More
Makala ya siha njema inaangazia kuhusu lishe bora na umuhimu wake katika jamii,hivi karibuni ripoti ya shirika la afya la kimataifa imebainisha kuwa mtu mmoja hufariki dunia katika watu watano kwa kukosa lishe bora.Daktari Lucas Mkeni wa Dar es salaam Tanzania analiangazia hili...

Duration:00:09:12

Fahamu Juu ya Chazo,Dalili na Tiba ya Mambukizi Katika Njia ya Mkojo (U.T.I)

1/16/2017
More
Neno U.T.I ambalo ni ni kifupisho cha Urinary Tract infections,ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo si geni katika masikioni mwa wengi, Ni tatizo kubwa ambalo hivi karibuni limetajwa kusumbua zaidi watoto wa kike na wanawake haswa kwa wanafunzi wanaotumia vyoo vya jumuiya. Basi leo kwa mara nyingine kupitia Makala yetu ya Siha Njema tutazungumzia juu ya tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo Urinary Tract Infection,tatizo ambalo hivi karibuni linawasumbua sana watoto na...

Duration:00:10:53

Fahamu Juu ya Chanzo na Tiba ya Tatizo la Moyo

1/2/2017
More
Kwa Mujibu wa Ripoti mpya za shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa ugonjwa wa shinikizo la damu ndio ugonjwa ambao unaathiri watu wengi zaidi barani Afrika huku ikionesha asilimia zaidi ya 10 ya Waafrika wameshapata na ugonjwa huo. Huku sababu kubwa zikitajwa kutokana na watu wengi hivi karibuni kupuuza kufanya mazoezi, kupunguza au kutotumia kabisa matunda angalau matano na mboga kwa siku, matumizi ya tumbaku au sigara na pombe Kipindi cha Siha Njema kwa juma hili kinangazia juu ya...

Duration:00:09:21

Sehemu ya Pili:Fahamu Athari za kiafya zitokanazo Mimba za Utotoni

10/31/2016
More
Nchi ya Uganda na Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo hutajwa kuongoza kwa mimba na ndoa za utotoni, hii ni kwa mujibu wa moja ya Shirika la Haki za Binadamu duniani. Licha ya kuwepo na jitianda mbali mbali katika nchi za afrika Mashariki na Kati za kupambana na ndoa za utotoni,lakini bado tatizo hilo limendelea kushamiri katika jamii zetu,hali ambayo imesababisha wanaharakati ya Afya na haki za binadamu kulalamikia mfumo mzima wa kusimamia sheria kwa kutowachukulia hatua kali za kisheria...

Duration:00:10:28

Fahamu Chanzo na Athari ya Mimba za Utotoni

10/24/2016
More
Tatatizo la Ndoa na mimba za utotoni limekuwa likiongezeka kila mwaka na kutajwa kusababisha umaskini mkubwa katika familia na mataifa mengi katika bara la Africa. Lakini Vile Vile tatizo hili la mimba za Utotoni limekuwa likichangia vifo vya mabinti wengi katika jamii zetu . Siha Njema kwa Jumaa hili kinagazia juu ya Chanzo na Athari za Mimba za Utotoni

Duration:00:10:50

Fahamu Juu Chanzo, Dalili na ya Ugonjwa Hatari wa Kisukar

10/17/2016
More
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Huku Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Na kwamujibu wa uchunguzi uliofanywa na jopo la madaktari bingwa kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 ulibaini asilimia 79 ya watanzania wazee waligundulika kuugua magonjwa ya kisukari. Basi kupitia kipindi chetu cha Siha Njema kwa mara nyingine kwa juma hili nitaweza...

Duration:00:09:21

Fahamu ya Pili:Fahmahu Ugonjwa wa Hatari wa Saratani kwa Watoto

9/12/2016
More
Ugonjwa wa Kansa au kwa jina jingine, Saratani,umetajwa kusababishia mwili madhara pale inapoharibu seli na kuzifanya zigawanyike bila kudhibitika na kuwa uvimbe wa tishu unaojulikana kama tumo Katika Sehemu ya pili na ya mwisho ya Makala yetu ya Siha Njema tunangazia juu ya Tiba ya Saratani na Naama Asasi isiyo ya kiserikali ya Marafiki wa Watoto wenye Saratanina mengine yanavyopambana na Ugonjwa huo hatari

Duration:00:11:04

Sehemu ya Kwanza:Fahamu Juu La Tatizo ya Saratani ya Watoto

9/5/2016
More
Ugonjwa wa Kansa au kwa jina jingine, Saratani, ni kundi la magonjwa yanayosababishwa na mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu za mwilini. Na hivi karibuni tumeshudia ongezeko kubwa la visa vya saratani barani Afrika vinavyosababishwa na maradhi mengine, Kipindi chetu cha Siha Njema kwa Juma hili nitatupia jicho juu ya Ugonjwa huu hatari

Duration:00:10:43

Fahama Juu ya Tatizo la Msongo wa Mawazo, Dalili Na Tiba Zake

7/25/2016
More
Tatizo la Msongo wa Mawazo (stress) au Mfadhaiko kama wengi walivyozoea ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi hivi karibuni,haswa watu wanoishi maeneo ya mijini Hali hii imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha afya na kusababisha vifo vya watu wengi vingi Basi kupitia Makala ya Siha Njema kwa jumaa hili itatupia jicho kuangazia juu ya Tatizo la Msongo wa Mawazo, Dalili Na Tiba Zake

Duration:00:09:19

Fahamu juu ya Uvumbuzi wa teknolojia ya Chujio Maalum la Kutibu na kuondoa Kemikali Kwenye Maji

7/18/2016
More
Ukosefu wa kwa huduma ya maji safi na salama mijini na vijijini kunasababisha wananchi wengi kutumia maji yasiyo salama, ambayo ni chanzo cha magonjwa kama kipindupindu. Kipindi chetu cha Siha Njema kwa jumaa hili kinagazia juu ya uvumbuzio wa teknolojia mpya ya Dr Askwar Hilonga,Chujio maalum la maji ambayo linatumia kuua wadudu na kuondoa chemikali mbali mbali zilizoko kwenye maji.

Duration:00:11:11

Chanzo na Tiba ya Maumivu Makali ya Tumbo wakati wa Hedhi (dismenorrhea)

6/20/2016
More
Tatizo la Maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea,ni changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua Wanawake wengi wakati wa hedhi , Maumivu haya hujitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati yai likiwa linatoka katika mirija ya ovari katika kizazi cha mwanamke na katika wakati huu uwezo wako wa kushika mimba Makala ya Siha Njema inagazia Juu ya Chanzo na Tiba ya Tatizo Maumivu wakati wa hedhi

Duration:00:09:53

Tatizo la Moyo na Tiba Yake

6/9/2016
More
Tatizo la Moyo Kupanuka au kuwa Mkubwa ni Tatizo ambalo limendelea kuathiri watu wengi hivi karibuni katika Kajamiii Zetu Tatizo hili linatokana na moyo kupanuka,wengine huzaliwa nalo,kudhoofu kwa misuli ya Moyo na sababu nyingine.Makala yetu ya Siha Njema tunaangazia juu ya Dalili na Tiba ya maradhi ya hayo

Duration:00:09:58