Wimbi la Siasa-logo

Wimbi la Siasa

RFI France

More Information

Location:

United States

Genres:

Podcasts

Networks:

RFI France

Language:

English


Episodes

Rais Joseph Kabila kubadilisha Katiba kuwania tena urais ?

5/30/2018
More
Kuna dalili kuwa rais Joseph Kabila wa DRC anapanga kuibadilisha Katiba ili kuwania urais kwa muhula wa tatu. Mabango ya picha ya rais Kabila, yaliyo na maandishi "Huyu ndio mgombea wetu" yameonekana jijini Kinshasa. Hii inamaanisha nini ? Tunajadili.

Duration:00:10:16

Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI yapata mitambo ya kuwatambua wapiga kura

2/22/2018
More
Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, imepata mitambo ya kieletroniki kuwatambua wapiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba. Je, mitambo hii itsaidia Uchaguzi huo kuwa huru na haki ? Tunajadili hili na mbunge wa Francois Rubota kutoka muungano unaomuunga mkono rais Joseph Kabila, Majorite Preidentielle, lakini pia Naibu Katibu Mkuu wa chama Kikuu cha upinzani UDPS Reubens Mikindo.

Duration:00:10:04

Kenya yaendelea kushuhudia mzozo wa kisiasa

1/10/2018
More
Kenya imeendelea kushuhudia mzozo wa kisiasa, baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita. Kiongozi wa upinzani NASA Raila Odinga, amekataa kumtambua rais Uhuru Kenyatta na amesema ataapishwa kama rais wa watu tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu. Je, kuna nafasi ya mazungumzo katika mzozo huu.

Duration:00:09:34

Maandamano ya Nchi ya Iran na amna Mataifa ya Magharibi Yalivyo na Mkono

1/3/2018
More
Makala ya Wimbi la Siasa Juma Hili Inaangazia Hali ya Kisiasa Nchini Iran Ambayo Kwa Majuma Kadhaa Imeshuhudia Maandamano ya Wananchi Wakipinga Hali Ngumu ya Maisha. Hata Hivyo Juma Hili Pia Wafuasi Wanaoiunga Mkono Serikali Nao Walifanya Maandamano Kuonesha uungaji Mkono Wao Kwa Serikali. Nini Hatma ya Siasa ya Nchi ya Iran? Ni Kweli Nchi za Magharibi Zina Mkono na Vurugu Zilizoshuhudiwa Iran?

Duration:00:09:52

Matukio makubwa ya kisiasa mwaka 2017

12/27/2017
More
Mwaka 2017, ulikuwa na mwaka wa kisiasa hasa barani Afrika. Uchaguzi tata nchini Kenya, siasa za Uchaguzi nchini DRC, Gambia kumpata rais mpya, Robert Mugabe kujiuzulu baada ya kuongoza Zimbabwe tangu 1980 na wabunge nchini Uganda kubadilisha Katiba. Tunakukumbusha mambo yalivyokuwa.

Duration:00:10:26

Wabunge nchini wabadilisha Katiba

12/20/2017
More
Wabunge nchini Uganda, wamebadilisha Katiba ya nchi hiyo kwa kuondoa kikomo cha mtu anayetaka kuwania urais nchini humo kutoka miaka 75. Hii inampa nafasi rais Yoweri Museveni kuwania tena urais mwaka 2021, akiwa na miaka 76. Upinzani umesema utakwenda Mahakamani kupinga mabadiliko hayo.

Duration:00:10:06

Nkurunziza azindua kampeni ya kuibadilisha Katiba

12/13/2017
More
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amezindua kampeni ya kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo, lenye lengo la kuongeza muda wa rais kukaaa madarakani kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Iwapo mabadiliko hayo yatapitishwa, Nkurunziza ana nafasi ya kuwania tena uongozi wa nchi hiyo mwaka 2020 na kuongoza mihula miwili hadi 2034. Hii ni mbinu ya Nkurunziza kuendelea kukaa madarakani ?

Duration:00:10:15

Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya kuamua hatima ya ushindi wa Kenyatta

11/8/2017
More
Mahakama ya Juu nchini Kenya inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi za kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017 ukidaiwa kuwa haukuwa huru, haki na wa kuaminika. Swali ni je majaji wa mahakama hiyo watafuta tena uchaguzi kama ilivyokua katika uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu ? Makinika na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata uchambuzi wa kina.

Duration:00:09:59

Ziara ya Rais Salva Kiir nchini Sudani na changamoto za mgogoro wa kisiasa

11/1/2017
More
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir hivi karibuni alifanya ziara nchini Sudan Kharthoum na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Omar Al Bashir wakilenga kuimarisha uhusiano na kuondoa hali ya wasiwasi baina ya pande hizo mbili kutokana na kushutumiana mara kwa mara kila upande ukilaumu upande mwingine kwa kusaidia waasi. Ziara hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa mgogoro wa Sudani Kusini? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa kujua mustakabali wa Sudani Kusini.

Duration:00:10:02

Mahakama Kuu nchini Kenya yataka wagombea urais kushiriki uchaguzi

10/11/2017
More
Hivi karibuni Mahakama Kuu nchini Kenya iliamua wagombea wote wanane wa urais washiriki katika uchaguzi wa marudio unaotarajiwa Oktoba 26 mwaka huu hatua ambayo imeibua maswali lukuki huku Muungano wa Upinzani NASA chini ya kinara wake Raila Odinga ukitangaza kujiondoa katika marudio. Kutokana na hali hiyo Kenya iko njia panda na kujua kwa undani mustakabali wa nchini na sheria zinasema nini? sikiliza Makala haya ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile.

Duration:00:10:13

Kenyatta achaguliwa tena Kenya upinzani wakimbilia mahakamani kupinga matokeo

8/16/2017
More
Uchaguzi mkuu wa Kenya ulifanyika hivi karibuni na Rais Uhuru Kenyatta kutangazwa kuwa rais mteule lakini upande wa upinzani umekimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo ukidai kufanyika udanganyifu. Je nini mustakabali wa nchi ya Kenya baada ya uchaguzi huo? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa mada hiyo.

Duration:00:10:15

Kampeni za lala salama zapamba moto nchini Kenya

8/2/2017
More
Kampeni za lala salama nchini Kenya zimepamba moto kuelekea uchaguzi huo Agosti 8 mwaka huu huku wagombea Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilei na mgombea wa NASA, Raila Odinga wakichuana vikali katika kinyang'anyiro hicho. Je nani atashinda katika uchaguzi huo na kwa nini? Uchambuzi wa kina katika Makala ya Wimbi la Siasa ukiwa naye Victor Robert Wile utakata kiu yako ya kujua mbivu na mbichi kuhusu uchaguzi wa Kenya.

Duration:00:10:19

Tume huru ya Uchaguzi Kenya na mchakato wa kutangaza matokeo

7/26/2017
More
Uchaguzi wa Kenya unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mchakato wa kutangaza matokeo huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, IEBC ikijinadi kuwa ina mamlaka ya kutangaza matokeo ya mwisho licha ya matokeo kutangazwa katika vituo na majimbo ya kupigia kura. Unajua ni kwa nini IEBC inatoa msimammo huo? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kujua kwa undani.

Duration:00:10:00

Umoja wa Mataifa waonya hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati

6/14/2017
More
Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulisema kuwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inabiliwa na ombwe kubwa la kiusalama na kwamba jitihada zaidi zinahitajika ili kusaidia nchi hiyo kuepuka kurudi ilikotoka. Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa mada hii.

Duration:00:10:01

Uchaguzi DRC bado njia panda

6/7/2017
More
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia, DRC Joseph Kabila alisema kuwa hajawahi kuahidi kuwa uchaguzi utafanyika lini na akasisitiza kuwa uchaguzi bora utafanyika na si bora uchaguzi katika mazingira ya amani na usalama. Je wajua mustakabali wa uchaguzi wa DRC? ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa kupata kinaga ubaga cha suala hilo.

Duration:00:09:59

Ufaransa watakavyomkumbuka Fraoncois Hollande

5/10/2017
More
Francois Hollande aliyekua rais wa Ufaransa amemaliza muda wake na kuiaga Ikulu ya Ufaransa na kumwachia kijiti Rais mpya Emmanuel Macron ambaye sasa anachkua usukani wa kuiongoza nchi hiyo. Pamoja na kuondoka kwake Francois Hollande historia ya nchi hiyo itamweka katika kumbukumbu. Je rais huyo wa mstaafu atakumbukwa kwa yapi? Fuatilia Makala haya ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile kupata undani wa mada hivyo.

Duration:00:10:10

Tofauti za kisiasa kumalizwa nchini Uganda

4/2/2017
More
Serikali ya Sweden iko tayari kuingilia kati mvutano wa kisiasa nchini Uganda na kuwasuluhisha wanasiasa wanaotofautiana yaani Rais Yoweri Museveni na mpinzania wake Kiiza Besigye. Je jitahada hizo zinaweza kuwa mwarobaini kile kinachoendelea nchini Uganda? Ungana na Victor Robert Wile kupata undani wa mada hiyo katika Makala ya Wimbi la Siasa.

Duration:00:10:04

Serikali ya Burundi kugomea mazungumzo na hatima ya nchi

2/15/2017
More
Mazungumzo ya amani ya Burundi yanaendelea kusuasua baada ya Serikali ya nchi hiyo kukataa kushiriki mazungumzo yaliyoitishwa Mjini Arusha na Mratibu wa usuluhishi na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa. Nini hatima na mustakabali wa baadaye wa Burundi? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa hapa RFI Kiswahili kupata majibu ya swali hilo.

Duration:00:09:59

Rais mpya wa Gambia akabiliwa na changamoto

1/25/2017
More
Rais mpya wa Gambia amerejea nchini mwake kutoka nchini Senegal alikokimbilia baada ya hali ya kisiasa kuchafuku wakati Yahya Jammeh alipogoma kuachia madaraka ya Urais baada ya kushindwa. Kutokana na hali hiyo Rais Adama Barrow anakabiliwa na changamoto lukuki za kiutawala. Ungana na Victor Robert Wile katika makala ya Wimbi la Siasa kufahamu mengi zaidi.

Duration:00:09:58

Obama na Trump watofautiana kiutawala

1/11/2017
More
Kuondoka madarakani kwa Rais wa Marekani Barack Obama na kuingia madarakani kwa Donald Trump kumeibua mitizamo na hisia tofautitofauti miongoni mwa wananchi wa Marekani. Je sura ya Marekani kiutawala itaelekea katika mkondo gani baada ya utawala wa Obama kutamatika, ungana na Victor Robert Wile katika makala ya Wimbi la Siasa kupata undani mustakabali wa Marekani.

Duration:00:10:09