Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Rein Paulsen: Wakati wa kuchukua hatua kuepusha baa la njaa Sudan ni sasa

4/22/2024
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Sabrina Moshi anasimulia.

Duration:00:03:27

Ask host to enable sharing for playback control

DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani

4/22/2024
Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu. “Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzitumia vyema na kuzisambaza, lakini sio jambo la maana kwani kitendo hicho ni kusema tuna sawazisha hali mbaya zaidi ya Kivu Kaskazini ni kwamba tunapaswa kupungua, inaweza kuwa ituri au Kivu Kusini. Hayo pia ni maamuzi magumu kwa sababu kuna watu wengi ambao hawana uhakika wa chakula katika maeneo hayo pia.”Bi.Jones amesema pamoja na kuwa na fahari na kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia wakimbizi wengi hapo awali, mtiririko mkubwa wa wakimbizi wanaowasili kusaka hifadhi katika makambi katika miezi ya hivi karibuni umefanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.

Duration:00:01:49

Ask host to enable sharing for playback control

22 APRILI 2024

4/22/2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya hali ya joto dunianina madhara yake kwa afya na wafanyakazi, Naomi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa ndani DR Congo. Makala tunakupeleka nchini Sudan na mashinani nchini Sudan Kusini, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa.Na mashinani tutapeleka Tambunra nchini Sudan Kusini kumsikia mkimbizi wa ndani akisihi kurejea kwa amani illi aweze kurudia nyumbani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:12:00

Ask host to enable sharing for playback control

ILO: Joto la kupindukia linaathiri asilimia 70 yawafanyakazi kote duniani

4/22/2024
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Asante Anold, akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Manal Azzi, afisa wa masuala ya usalama kazini na afya wa shirika la ILO amesema takwimu hizi za kustaajabisha zinasisitiza haja kubwa ya kurekebisha hatua zilizopo za usalama na afya kazini ili kushughulikia ipasavyo vitisho vinayojitokeza kutokana na hatari zinazohusiana na changamoto za hali ya hewa.Ameongeza kuwa “Zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wetu wanakabiliwa na joto jingi, angalau joto la kupindukia, katika wakati mmoja wa maisha yao ya kazi. Hiyo ni jumla ya wafanyakazi bilioni 2.4 duniani kote, kati ya wafanyakazi wa kimataifa wa bilioni 3.4.”Ripoti hiyo iliyopewa jina “Kuhakikisha usalama na afya kazini katika mazingira yanayobadilika” inaeleza kwamba mabadiliko ya tabianchi tayari yameleta athari kubwa kwa usalama na afya ya wafanyakazi katika kanda zote duniani.Kwa mujibu wa ILO waafanyakazi, hasa wale walio katika maeneo yenye umaskini zaidi duniani, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi kama vile joto kali, ukame wa muda mrefu, moto mkubwa wa nyika, na vimbunga vikali.Bi. Azzi amesema "Wafanyakazi zaidi ya milioni 22 wanaugua magonjwa na majeraha yanayohusiana na joto kali na haya yanaweza kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ajali katika usafiri, katika ajali za barabarani kutokana na usingizi kwa kutolala vizuri usiku kwa sababu kulikuwa na joto kupita kiasi, hadi ajali za ujenzi, majeraha, kuteleza na kuanguka. kunkohusiana na ongezeko la joto kali."Ripoti hiyo inabainisha kuwa baadhi ya athari za kiafya kwa wafanyakazi zilizohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, ni pamoja na saratani, ugonjwa wa moyo na mishipa, magonjwa ya kupumua, figo kuharibika na hali ya afya ya akili. Pia kuongezeka kwa joto na unyevu wa hali ya juu, dawa nyingi za wadudu hutumiwa katika sekta ya kilimo na kufanya wafanyikazi milioni 870 katika kilimo kuwa na uwezekano wa kuathiriwa na viuatilifu, huku kukiwa na zaidi ya vifo 300,000 vinavyohusishwa na sumu ya dawa hizo kila mwaka.Bi Azzi amesisitiza kuwa mambo haya yote yanaingiliana na kwamba zana zinazofaa zinapaswa kuwepo ili kupima athari na kuwa na uwezo wa kufanyia kazi mapendekezo.Mkutano mkuu umepangwa kufanyika 2025 na ILO kwa kushirikisha wawakilishi wa serikali, waajiri na wafanyakazi ili kutoa mwongozo wa sera kuhusu hatari za mabadiliko ya tabianchi katika masuala ya kazi.

Duration:00:02:58

Ask host to enable sharing for playback control

Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT

4/20/2024
Lugha ni miongoni mwa njia za kimsingi za kujenga utangamano duniani. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa lugha ni chombo cha kusongesha tamaduni na miongoni mwa lugha zilizotengewa siku mahsusi kusherehekewa ni kichina ambacho shamrashamra zake ni tarehe20 mwezi Aprili ya kila mwaka.Lugha hii imesambaa duniani ikiwemo Tanzania ambako hii leo Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki amefuatilia mafunzo yake kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.

Duration:00:05:18

Ask host to enable sharing for playback control

Joram Nkumbi na Vivian Joseph: Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza toka kwa wenzetu

4/19/2024

Duration:00:03:19

Ask host to enable sharing for playback control

Francesco La Camera: Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kuhamia haraka katika nishati jadidifu

4/19/2024

Duration:00:02:27

Ask host to enable sharing for playback control

19 APRILI 2024

4/19/2024
Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Duration:00:14:40

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhiri na hadhiri.”

4/18/2024
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na hadhiri.”

Duration:00:01:11

Ask host to enable sharing for playback control

18 APRILI 2024

4/18/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na hadhiri."Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023. Mkutano wa Wiki ya Uendelevu ya Umoja wa Mataifa unaendelea hapa Makao Makuu New York Marekani, leo ukijikita na mada ya miundombinu endelevu na inayoaminika ambayo Umoja wa Mataifa unasema itazisaidia nchi kuelekea kwenye maendeleo yenye miumbombinu bora, isiyo ya hatari na itakayoongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na hadhiri.”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:11:34

Ask host to enable sharing for playback control

Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

4/17/2024
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..

Duration:00:08:35

Ask host to enable sharing for playback control

Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk

4/17/2024
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi jimboni Ituri. Taswira ya angani kutoka ndege hii ya Umoja wa Mataifa na kisha wanawasili. Mapokezi hapa Bunia, kutoka kwa wenyeji wao.Moja kwa moja msafara wao wa magari unafika kwenye kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji wa Bunia na wanaingia ndani ambako wanawake, wanaume na watoto, wazee na vijana, nyuso zao zinaonesha matuamini kwani wahenga walinena mgeni njoo mwenyeji apone.Mkalimani akamweleza Turk kuwa wanachosema maeneo yao yametawaliwa na waasi na hawawezi kurejea makwao.Na ndipo Kamishna huyu Mkuu wa Haki za Binadamu baada ya kuwasikiliza wakimbizi na kuzungumza nao akatoka nje na kusema, “Nimekutana na kundi la watu ambao wamefurushwa makwao kutokana na mauaji ya kikatili na ya kutisha yaliyotekelezwa kwenye makazi yao. Na wamekuweko hapa kwa miaka minne sasa. Tamanio lao kubwa kabisa ni kuweza kurejea makwao.”Kwa sasa kuna takribani watu milioni 1.8 waliofurushwa makwao jimboni Ituri kati ya wakimbizi wote wa ndani milioni 7.2 nchini kote DRC.Kesho Bwana Turk atakuwa na mazungumzo na Rais President Félix Tshisekedi na maafisa wengine wa serikali, Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na vyama vya siasa pamoja na watetezi wa haki za binadamu na kisha atazungumza na waandishi wa habari.

Duration:00:02:31

Ask host to enable sharing for playback control

17 APRILI 2024

4/17/2024
Hii leo jaridani tunaangazia ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jitihada za Umoja wa Mataifa za kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunaelekea nchini Madagascar, kulikoni?Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukkwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania.Na mashinani tutakupeleka nchini Madagascar kusikia ujumbe kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini kwanza ni makala.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:13:01

Ask host to enable sharing for playback control

Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia

4/17/2024
Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu. Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati wa msimu wa muwambo kati ya mwezi Julai na Septemba.Viwango vya utapiamlo katika sehemu za Afar, Amhara, Tigray na mikoa mingine vinatia wasiwasi mkubwa na vinaendelea kuwa vibaya zaidi. Wakati huo huo, migogoro katika Tigray na mikoa mingine imeharibu maelfu ya shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya jamii.Mama huyu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni wa eneo la Afar, mashariki mwa Ethiopia ambako pia kumeathiriwa na mafuriko anapaza sauti akisema, “Ninataka kulea na kusomesha watoto wangu vizuri. Nawatakia watoto wangu mema.”Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wanaunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kuongeza msaada wa kuokoa maisha kwa watu milioni 15.5, na msaada wa chakula kwa watu milioni 10.4 nchini humo Ethiopia. Kwa mwaka mzima, ili mpango huo ufanikiwe unahitaji dola za Marekani bilioni 3.24.

Duration:00:01:56

Ask host to enable sharing for playback control

16 APRILI 2024

4/16/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete. Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo.Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 ya kibinadamu, ya maendeleo na serikali wametoa ombi la haraka la dola milioni 112 ili kuwasaidia zaidi ya wahamiaji milioni 2.1 na jamii zinazowahifadhi. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na jamii hizo ni katika njia za uhamiaji za Mashariki na Kusini zkijumuisha Djibouti, Ethiopia, Somalia, Yemen, Kenya na Tanzania.Na mashinani leo tunakwenda mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususan jimboni Ituri ambako huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umechukua hatua kukabili mashambulizi kutoka waasi, mashambulizi ambayo kila uchao yanazidi kufurusha raia. Mzungumzaji wetu ni Luteni Kanali Mensah Kedagni, msemaji wa kijeshi wa MONUSCO.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:12:09

Ask host to enable sharing for playback control

Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

4/15/2024
Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.

Duration:00:03:03

Ask host to enable sharing for playback control

Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa

4/15/2024
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis. Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili. Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili.Mwenyekiti wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusuu watu wa asili Bi. Hindou Oumarou Ibrahim akizungumza katika jukwaa hilo amesema “Kuondolewa vikwazo kwenye upatikanaji wa fedha ni muhimu ili kuhakikisha watu wa asili wanatekeleza kwa vitendo mipango yao na kuwa na njia ya kudumisha kujitawala,” Kwa upande wake Bwana Li Junhua, ambaye ni msaidizi waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) amesema “unahitaji ufadhili wa muda mrefu, unaotabirika, na wa moja kwa moja kwa Watu wa Asili, ikijumuisha kupitia mifumo ya ufadhili ya umma, ya kibinafsi, na inayoongozwa na Wenyeji ambayo inashirikisha kikamilifu Wanawake na vijana wa kiasili.”Unaweza kufuatilia moja kwa moja matangazo ya jukwaa hili yanayorushwa mubashara na Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake wa UN Web TV,matangazo yanarushwa kwa lugha rasmi sita za umoja wa Mataifa ambazo ni Kingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.

Duration:00:01:53

Ask host to enable sharing for playback control

15 APRILI 2024

4/15/2024
Hii leo jaridani tunaangazia utekwaji nyara wa watoto wa kike 275 huko Chibok nchini Nigeria, na uwezeshaji kiuchumi wa watu wa asili. Makala inamulika masuala ya mazingira ikiangazia watut wa asili na mchango wao, na mashinani tunakupeleka nchini Chad kusikia simuliza ya mkimbizi kutoka Sudan. Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Makala Stella Vuzo, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, anatuletea mazungumzo kati yake na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhudhuria wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika mwezi uliopita jijini Nairobi, Kenya. Kwa kuwa jamii zinazoishi kiasili wakati mwingine zimekuwa zikilaumiwa kuwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.Na mashinani tunamulika vita nchini Sudan ambayo inaendelea kuwalazimisha mamilioni ya watu kukimbia kuokoa maisha yao. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mkimbizi ambaye alikimbia machafuko nchini humo kuelekea Chad anasimulia changamoto alizozipitia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:11:05

Ask host to enable sharing for playback control

UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi

4/15/2024
Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi. Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa. Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiingereza, inaonesha ukweli mchungu wa kufanikisha safari hiyo kwa mtoto nchini Nigeria kuweko shuleni bila uoga. Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Cristian Munduate amesema tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok ni kengela ya kutuamsha juu ya hatari kubwa watoto wetu wanakabiliwa nayo wanaposaka elimu. Anasema leo tunapotafakari janga hili na mengine ya hivi karibuni ni dhahiri kuwa juhudi zetu za kulinda mustakabali wa watoto wetu lazima ziimarishwe. Mwakilishi huyo anasema kwa kuzingatia takwimu zilizotolewa na ambazo zinatia hofu kubwa, ni lazima kupata majawabu ya sio tu dalili bali pia chanzo cha janga hilo la utekaji nyara watoto. Bi. Munduate amekumbusha kuwa elimu ni haki ya msingi na ni njia muhimu ya kuelekea kuondokana na umaskini. Lakini kwa watoto wengi nchini Nigeria inasalia kuwa ndoto isiyotimizika. Ripoti ilimulika maeneo 6 ikiwemo mifumo thabiti ya shule, ukatili dhidi ya watoto, majanga ya asili,mizozo ya kila siku na miunmdombinu ya shule na kubaini utofauti mkubwa wa vigezo hivyo katika majimbo yote 36. Jimbo la Borno liko thabiti kwani limekidhi viwango kwa asilimia 70 ilhali majimbo ya Kaduna na Sokoto bado yako nyuma. Uchambuzi huu unakuja wakati kuna ripoti za ongezeko la ghasia dhidi ya shule ambapo katika miaka 10 iliyopita, matukio ya mashambulizi yamesababisha watoto zaidi ya 1,680 kutekwa nyara wakiwa shuleni au kwinigneko. UNICEF inataka Nigeria pamoja na mambo mengine ihakikishe shule kwenye majimbo yote zina rasilimali za kutekeleza MSSS. Pia itatue pengo la uwiano wa usawa katika hatua za kuimarisha usalama shuleni. Nigeria pia iimarishe usimamizi wa sheria na mikakati ya usalama ya kulinda taasisi za elimu na jamii dhidi ya utekwaji. Kwa sasa UNICEF inashirikiana na serikali kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mazingira salama ya kusomea. Soma ripoti nzima hapa.

Duration:00:02:58

Ask host to enable sharing for playback control

Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo

4/12/2024
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona. Tukio lilianza kwa ukumbi kuwa giza na video ya dakika tano ikachezwa kueleza kuwa watu wengi wanaijua Rwanda kuanzia 1994, lakini ilikuweko hata kabla ya ukoloni, na kwamba wakoloni ndio waligawa watu kwa misingi ya makundi licha ya kwamba lugha yao ilikuwa moja. Manusura na watekelezaji wa mauaji walizungumza pia kwenye video hiyo!Video ikafuatiwa na kuwasha mishumaa kukumbuka waliouawa na kisha hotuba ambapo Katibu Mkuu Guterres akawa ana ujumbe mahsusi kwa vijana wa Rwanda walioshiriki kimtandao na pia ukumbini.Anasema rafiki zangu, katu hatutasahau vitisho vya siku 100. Lakini tunahitaji msaada wenu. Tunahitaij sauti na uchechemuzi wenu kusongesha kumbukizi za wale waliouawa. Na kukemea chuki kokote muisikiako au muionapo. Mijini kwenu, vitongojini, shuleni, mtandaoni, popote pale na kila mahali.Akaendelea kusema kuwa hebu na tuondoe chuki na ukosefu wa stahmala kokote tuvionapo. Kumbukumbu za waliouawa zichochee vitendo vyetu, na azma yetu ya kuhakikisha dunia bora na salama kwa watu wote. Guterres amesema Umoja wa Mataifa kila wakati utashikamana na vijana katika juhudi hizo muhimu. Mauaji ya kimbari Rwanda ya mwaka 1994 yalifanyika kwa siku 100 kuanzia tarehe 7 Aprili na zaidi ya watu milioni moja waliuawa, wengi wao Watutsi, halikadhalika wahutu wenye msimamo wa kati na watu wengine waliokuwa wanapinga mauaji hayo. Katibu Mkuu amesema siku hizo 100 ziliakisi ubaya zaidi wa ubinadamu. Lakini kipindi baada ya mauaji kilidhihirisha ubora wa roho ya ubinadamu: mnepo, maridhiano, ujasiri na nguvu. Amesema simulizi za manusura ni ushahidi wa nguvu ya matumaini na msamaha ambapo amemtaja manusura Laurence Niyonangira ambaye alipoteza jamaa zake 37 wakati wa mauaji hayo. “Alichagua kusamehe mmoja wa wahusika wa mauaji ya familia yake baada ya mhusika kuungama na kutumikia muda jela kwa makosa aliyotenda. Kama manusura, Laurence alisema ‘tunaweza kuponya vidonda kwa kushirikiana wale waliovisababisha.” Amesema Guterres. Hivyo Katibu Mkuu amesema mwaka huu ambapo kumbukizi inajikita kwenye mzizi wa mauaji ya kimbari ambao ni chuki, ambayo sasa inakolezwa na mitandao ya kijamii, “ni lazima tushikamane pamoja na kurejelea shinikizo la dunia la kuridhia na kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya kimbari, huku tukiimarisha mifumo ya kuzuia, kuelimisha vizazi vipya kuhusu mauaji ya kimbari yaliyopita na kukabili taarifa potofu na za uongo ambazo huchochea kauli za chuki na nia na vitendo ya mauaji ya kimbari.”

Duration:00:03:37