Jua Haki Zako-logo

Jua Haki Zako

RFI

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Location:

United States

Networks:

RFI

Description:

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Language:

Swahili


Episodes
Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii

5/21/2024
Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica. Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au wale huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi. Kwa mjibu wa twakwimu za shirika la afya duniani WHO ni kwamba wanawake 15 kati ya 100 barani Afrika hawana uwezo wa kupata watoto, na kati ya wanawake 6 angalau mmoja huwa hawana uwezo wa kupata mtoto kidunia. Swala la kukosa kupata mtoto hushuhudiwa kati ya wanawake na wanaume, ila hapa barani africa kasumbuka mara nyingi huelekezewa kina mama, hili likisababisa dhiki, unynyapaa, ufukara miongoni mwa wanawake wengi wao sasa wakiathiriwa na afya ya akili na hata kisaikolojia. Licha ya tatizo hili kuwa na suluhu, wengi wamesalia kukosa imani kutokana kwani hawana pesa za kutafuta tatibu husika. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

Duración:00:10:03

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

DRC : Makundi ya waasi yatuhumiwa kwa ukatili wa kijinsia dhidi ya raia mbilimo

5/18/2024
Nchini DRC ; familia ya jamii ya mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu. Wanawake na wasichana kutoka jamii hii wengi ni waathiriwa wa vitendo vya ubakaji , vinavyo tekelezwa na wanaume kutoka makundi ya waasi mashariki mwa DRC, visa hivi vina tendwa na wanaume . Mwezi Aprili mwaka huu kule mkowani Ituri, watetezi wa haki za binadamu walichapisha ripoti ilioashiria namna wasichana na wanawake mbilikimo , wamebakwa na wanapiganaji wa makundi ya waasi. Hali hii imedaiwa kuchochewa na imani potofu kwamba , ukitenda tendo la ndoa na mwanamke au msichana mbilikimo, huwezi kufariki kwa risasi vitani wala kuambukizwa baadhi ya magonjwa . Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

Duración:00:10:00

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?

5/9/2024
Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume. Wajiku Maina raia kutoka nchini Kenya, anasema katika jamii ya leo hakuna anayeshughulikia haki na majukumu ya mtoto wa kiume, hali ambayo imechangia kizazi kizembe cha mtoto wa kiume. Skiza makala haya kufahamu suluhu kwa baadhi ya changamoto za mtoto wa kiume.

Duración:00:09:54

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023

5/2/2024
Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi. Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika. Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya. Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

Duración:00:09:56

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

4/25/2024
Unamkumbuka kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya. Baada ya takriban mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki. Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi. Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi Katika haya mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa

Duración:00:09:51

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua

4/17/2024
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi. Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao. Makala haya yameandiliwa na Benson Wakoli Soma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

Duración:00:09:09

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao

4/16/2024
Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.

Duración:00:09:29

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

DRC : Jamii ya mbilikimo yalilia serikali kuwapa nafasi kuhudumu serikalini

4/10/2024
Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC. Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali. Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto. Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.

Duración:00:10:05

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Haki za raia wa mataifa ya Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya ughaibuni.

4/4/2024
Raia wa mataifa tofauti tofauti ya Afrika ikiwemo Kenya na Uganda huelekea katika mataifa ya kiarabu kutafta ajira Kila mwaka . Changamoto nyingi zikiripotiwa.Kwenye makala haya Florence amezungumza nao wakina dada wanaofanya kazi huko .

Duración:00:10:08

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Dhuluma za kijinsia na mrundiko wa kesi mahakamani

3/19/2024
Katika makala haya tujahadili dhuluma za kijinsia swala ambalo limekuwa ni donda sugu kwenye familia zetu, na jamii kwa ujumla. Wakili Latifa Njoki na wakili Elizabeth Njambi wote kutoka nchini Kenya wanafafanua swala la mrundiko wa kesi mahakani zinazohusiana na dhuluma za kijinsia na suluhu.

Duración:00:10:07

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

DRC: Waasi wa CODECO wadaiwa kutekeleza mauwaji ya kikabila

3/15/2024
Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi. Makundi haya ni yale ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" . Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika raia wakiwa hai. Makala haya yamlika hali wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia 800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .

Duración:00:10:07

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya: siku ya wanawake duniani nini Kipya?

3/8/2024
Siku ya wanawake duniani huadimishwa kila kila tarehe nane ya mwezi machi, kuangazia mchango wa mwanamke katika jamii na pia changamoto zinazowakumba wanawake. Kauli mbiu ya maadimisho ya mwaka huu, nchini Kenya ni uwekeza kwa wanawake ili kufanikisha maendeleo kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

Duración:00:09:17

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Wasanii walilia haki yao

3/2/2024
Muungano wa wanamziki nchini Kenya (MAAK), unamtaka mwenyekiti wa Shirika la Hakimiliki ya Muziki ya Kenya, Ezekiel Mutua kujiuzulu kutokana na kile wanadai amekuwa akipora peza za wamziki. Kupitia taarifa muungano huo, unasema Mutua amekuwa akijilimbikizia pesa za wasanii huku wahusika wakiendelea kusalia maskini. Ili kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duración:00:09:59

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Haki ya kutali Africa bila vikwazo

2/21/2024
Ni vigumu kwa watu wachache kutumia usafiri wa beskeli hapa Africa lakini Yusufu raia wa Morocco kwake kutali Africa kwa kuendesha beskeli ni kama kazi. Benson Wakoli aliketi chini na Yusuf, kuthamini safarizake barani Africa na jinsi gani amekuwa akipokelewa na raia wa mataifa mengine.

Duración:00:10:11

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Valentine : Haki ya wanaume na wanawake

2/17/2024
Kila mwaka Feb 12 dunia huadimisha siku ya wapendanao, raia wengine wakionesha mapenzi kwa wachumba, pamoja na marafiki. Lakini nini maana ya valentine? kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duración:00:09:56

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Kenya : Viongozi wa dini wapinga ushoga

2/9/2024
Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya. Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za kiafrica. Kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duración:00:10:00

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

DRC : Je haki za raia zilikiukwa kipindi cha uchaguzi?

2/3/2024
Katika makala haya tunapiga darubini kuangazia haki za raia wa DRC wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi, na baada ya uchaguzi. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mapendo Kusudi alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mwandishi wetu Benson Wakoli. Kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duración:00:10:00

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Haki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

1/26/2024
Katika haya tunaangazia haki ya watoto kupata elimu ambapo utaskia kwa wadau mbalimbali walioazisha kutuo cha elimu cha Fizi kinatoa elimu ya somo la kifaransa nchini Kenya kwa watoto wakimbizi kutoka nchini DRC , Rwanda na Burundi. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2014 lengo likiwa kuwasaidia watoto wakimbikizi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ili kuendelea kujifunza na kuendeleza tamaduni ya lugha ya Kifaransa,hasa ikizingatiwa kwamba nchini Kenya raia wengi huzungumza kingereza na Kiswahili.

Duración:00:10:00

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Human watch yatahumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kusadia Sudan

1/21/2024
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kushughulikia vita vinavyoendelea nchini Sudan. Kwa mjibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo, jamii ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushawishi pande hasimu nchini Sudan Kusitsha vita. Ili Kufahamu negi zaidi skiza makala haya.

Duración:00:10:00

Pídele al anfitrión que permita compartir el control de reproducción

Hali ya haki za binadamu nchini Kenya na Tanzania

1/9/2024
Visa vya raia kupotea na kisha kuonekana baada ya siku kadhaa nchini Kenya si vipya tena, hili likishuhudia mara kwa mara nchini Kenya, polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye visa hivi lakini je tume ya haki za binadamu nchini Kenya inafahamu hili? na je nchini Tanzania hali ya hali za haki za binadamu ipo je? Maswali haya yanajibiwa ndani ya makala.

Duración:00:09:46