
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Kenya: Mradi wa PLEAD Kenya yaleta mabadiliko chanya katika uwezeshaji wa kisheria
10/3/2025
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP
Duration:00:04:55
UN: Buriani Jane Goodall, mwanamazingira na mtaalamu wa sokwe
10/3/2025
Kufuatia kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani, halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Duration:00:02:49
03 OKTOBA 2025
10/3/2025
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya katika hospital Gaza, mradi wa PLEAD nchini Kenya na mafanikio yako katika kesi za mashinani, na kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP.Kufuatia kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani, halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:12:19
Gaza: Mashirika ya UN yaonya kuwa hospitali zimegeuka kuwa uwanja wa mapambano
10/3/2025
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali. Flora Nducha amefuatilia na hii hapa taarifa yake
Duration:00:02:58
Jifunze Kiswahili: Maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"
10/2/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"
Duration:00:00:47
02 OKTOBA 2025
10/2/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi neno la wiki.Haiti, hali ya kibinadamu imefika kiwango cha hatari, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk. Akihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Türk amesema Haiti imefika kiwango cha kulipuka kutokana na ukatili na ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu. Amesisitiza kuwa “Tunaweza na lazima kubadili hali hii kwa ajili ya watu wa Haiti,” akiongeza kuwa “bila hatua za haraka hali mbaya zaidi huenda ikaja kwa Haiti na eneo zima.”Tukielekea Mashariki ya Kati huko Gaza, janga la kibinadamiu linaongezeka ambapo mashambulizi yanayoendelea yameathiri vibaya upatikanaji wa chakula na maji. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, limeripoti kuwa usambazaji wa chakula kilichopikwa kaskazini mwa Gaza umepungua kwa asilimia 70, huku vituo vinne pekee ndivyo vinavyofanya kazi. Takriban watu milioni moja wanapata maji chini ya lita sita kwa siku, kiwango kilicho chini ya hali ya dharura.Nchini Sudan Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Volker Türk ameonya kuhusu hali katika mji wa El Fasher, Darfur Kaskazin , akisema mji huo “uko kwenye ukingo wa janga kubwa zaidi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kulegeza mzingiro wa kijeshi na kuwalinda raia,” huku Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kikiongeza juhudi za kutwaa mji huo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:11:08
Gaza - Matumizi ya plastiki kama nishati ya kupikia yasababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua
10/1/2025
Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu. Tuungane na Leah anayetujuza zaidi
Duration:00:02:49
Lazima tutambue mchango wa wazee katika kuunda jamii zenye haki - UN
10/1/2025
Tuanzie hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.
Duration:00:03:07
01 OKTOBA 2025
10/1/2025
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Wazee duniani na mchango wao kwa jamii, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na simulizi ya Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:11:29
Angelique Kidjo, Mwanamuziki, asimulia safari yake ya elimu akiunga mkono wito wa UNICEF kwa viongozi wa Afrika
10/1/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
Duration:00:03:22
EAC yasisitiza usalama, uchumi na masuala ya kidijitali katika Mjadala Mkuu wa UNGA80
9/30/2025
Kama unavyofahamu Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 umekunja jamvi rasmi jana Jumatatu. Na tumepata fursa ya kuzungumza na washiriki mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala huo kuangazia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ikiwemo masuala ya Amani na usalama, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Ungana nao.
Duration:00:09:11
30 SEPTEMBA 2025
9/30/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Ikiwa ni zaidi ya miaka minane tangu zaidi ya wakimbizi 750,000 waislamu wa kabila la warohingya wakimbie Myanmar kuelekea kwenye kambi kubwa nchini Bangladesh, mgogoro huo bado haujapatiwa suluhisho na leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa viongozi wamekutana kusaka suluhu ya kudumu kwa warohingya na makabila mengine madogo nchini Myanmar. Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia Afisa Mtawala Mkuu wa UN Courtenay Rattray amesema, “mgogoro huu, ambao umezidi kuongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi Myanmar ya mwaka 2021, unasigina haki za binadamu, utu na usalama wa mamilioni ya watu na unatishia uthabiti wa kikanda. Haitoshi tu kutathmini hali ilivyo. Tunapaswa pia kuendeleza mshikamano na kubuni suluhisho.”Amani nchini DRC imesalia bado ahadi, ni kauli ya Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama lililokutana leo kujadili hali Mashariki mwa DRC. Anasema hali inazidi kuwa tete. “Ghasia zinaendelea kushamiri jimboni Kivu Kaskazini hususan eneo la Rutshuru tangu waasi wa M23 watwae eneo hilo. Kuanzia mwezi Juni na kuendelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepokea maombi lukuki ya watu wakitaka ulinzi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na M23.”.Na mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamesisitiza wito wa kupatikana kwa sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, ili kupunguza machungu wakati huu ambapo Mpango wa Marekani wa Vipengele 20 unaibua matumaini ya kukomeshwa kwa mapigano. Ricardo Pires, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF amesema, “ni muhimu tupate sitisho la mapigano na misaada iweze sio tu kuingia na kuepusha baa la njaa, bali pia kuelekezwa maeneo ya kusini. Lakini vile vile kuhakikisha watoto na familia zao wanapata malazi bora wakati huu majira ya baridi kali yanakaribia. La sivyo italeta zahma ya afya kwa watoto na familia zao.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:12:03
Mizozo inayoendelea duniani, uchumi Afrika vyatawala siku ya mwisho ya mjadala mkuu
9/29/2025
Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.
Duration:00:03:03
Ili Afrika ‘iimarike kiafya’ inabidi isiwe tegemezi kwenye masuala ya kifedha: Dkt. Ntuli Kapologwe
9/29/2025
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masuala mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza tena na Dkt. Kapologwe mara tu baada ya mkutano huo
Duration:00:03:29
29 SEPTEMBA 2025
9/29/2025
Hii leo jaridani tunaangazia leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 tukimulika hotuba za viongozi na mikutano mingine ya pepmbezoni kuhusu malengo ya maendeleo enedelevu, SDGs.Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha.Tukisalia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masula mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:11:35
Afrika imedhamiria kuhakikisha ina sauti na nafasi Baraza la Usalama la UN: Balozi Lokaale
9/29/2025
Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha
Duration:00:03:04
UNGA80 na maelezo kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs - Dkt. Mohamed Yakub Janabi
9/26/2025
Mada hii kwa kina inamulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wazungumzaji wa Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi
Duration:00:07:43
VVU: Sindano ya kuzuia kupatikana kwa bei nafuu kuanzia mwaka 2027
9/26/2025
Makubaliano yaliyosimamiwa na mashirika ya kimataifa, likiwemo UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, halikadhalika Mpango wa afya wa Clinton (CHAI), Wits RHI na Maabara ya Dkt. Reddy, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa Lenacapavir kwa gharama nafuu.Dawa hii, inayodungwa mara mbili pekee kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, jambo muhimu hasa kwa wale wanaopata changamoto kutumia dawa za kila siku.Video ya UNITAID inaonesha maabara yenye teknolojia ya hali ya juu, ambamo wanasayansi wanaandaa dawa hiyo inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID, Tenu Avafia, anasema hatua hii ni ushindi mkubwa kwa jamii zinazohitaji kinga ya muda mrefu dhidi ya VVU."Tumeitikia wito kutoka kwa jamii na nchi tunazohudumia kwa kuhakikisha dawa hii inapatikana kwa gharama nafuu. Tunatarajia usambazaji wa toleo la bei nafuu la dawa hii kuanza kufikia mwaka 2027, chini ya miaka miwili tu tangu idhini kutolewa katika nchi za kipato cha juu — kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa."Akizungumza kuhusu hatua hii muhimu, Carmen Pérez Casas, Mkuu wa Mikakati Mwandamizi wa UNITAID, anasema:"Kwa kushirikiana na watengenezaji wa dawa mbadala, tumefanikisha bei nafuu mapema zaidi. Lakini bado tunahitaji kusaidia nchi na jamii kwa kuongeza upatikanaji."UNITAID inasema kwa msaada wa mashirika kama PEPFAR ambao ni mfuko wa Rais wa MArekani wa usaidizi wa dharura dhidi ya UKIMWI, pamoja na mfuko wa kimataifa na wakfu wa Gates, hatua hii inaleta matumaini ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU duniani.
Duration:00:02:17
Mwanaharakati Dkt.Owusu: Ni wakati wa sauti zetu vijana zisikilizwe kwa vitendo
9/26/2025
Katika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana wa Uingereza na Ghana, Dkt. Khadija Owusu ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili.Owusu, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Akaya inayowakilisha wasichana wa zama hizi, anasema vijana hawapaswi kuzungumziwa tu, bali wajumuishwe moja kwa moja katika kuandaa Suluhu za changamoto zinazoihusu dunia wakiwemo na wao "Mara nyingi tunazungumza kuwa tunataka ushiriki zaidi wa vijana wakati umefika wa kuacha kuzungumza tu kuhusu kuhitaji vijana wengi, bali tuwe na vijana wengi."Niko hapa kuwakilisha maelfu ya wasichanaAnasema ushiriki wake katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa vijana si wa kibinafsi tu, bali unaakisi sauti za wasichana na vijana wengi wanaosaidiwa na taasisi yake ya Akaya."Niko hapa kuwakilisha si mimi peke yangu, si Uingereza tu, na si Ghana tu, bali Taasisi ya Akaya, na wasichana na vijana wengi tunaowahudumia nchini kote."Owusu anaamini vijana wa Kiafrika, hususan wasichana, wanapaswa kupata nafasi kubwa zaidi katika jmaukwaa ya kimataifa kama Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kupaza sauti zao."Bado tunahitaji kuona vijana zaidi kama sisi kwenye vyumba vya mikutano, Waafrika zaidi, vijana zaidi wa Kiafrika na wasichana wa Kiafrika kwenye vyumba vya mijadala, wakishiriki majadiliano kwa sababu tunaleta mabadiliko halisi."Owusu anasema ujumbe wake kwa vijana barani Afrika ni kubeba vipaji vyao, wajiamini, na kuendeleza ndoto zao kwani kila kitu kinawezekana.
Duration:00:02:10
UNGA80:Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa
9/26/2025
Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Ilikuwa majira ya saa tatu na dakika chache hivi asubuhi ya leo saa za New York nchini Marekani ambapo Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu amepewa fursa ya kuhutubia na ndipo ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukakosa utulivu. Wajumbe kwa makundi walinyanyuka katika viti vyao na kuondoka huku wakiwaacha maafisa wa Israel wakimpigia makofi kiongozi wao na pia nchi zinazoiunga mkono Israel zikasalia katika viti vyao ikiwemo Marekani.Baadhi ya wajumbe watoka njeKatika eneo la walipotakiwa kukaa wawakilishi wa Palestina kulikuwa wazi, huku katika eneo la Iran ikibakia picha iliyokusanya sura za baadhi ya watu wao waliouawa na mashambulizi ya Israel. Bwana Netanyahu kwa mara nyingine tena ameingia na ubao wenye picha ya ramani ya eneo la Mashariki ya Kati akiutumia kuishambulia Iran na kwa kutumia kalamu akiweka alama ya vema kuonesha namna ambavyo Israel imefanikiwa kupambana na ngome za Irani katika ukanda huo. Katika suti yake, kifuani upande wa kulia, Bwana Netanyahu pia ameweka kibandiko chenye QR Code na akawaambia watu kuwa Israel bado inakumbuka tukio walilofanyiwa na Hamas mwezi Oktoba mwaka juzi na kwamba ikiwa watu wamesahau hilo basi waelekeze simu zao kwenye QR Code hiyo kwenye nguo yake ili iwaoneshe madhara yaliyofanywa na Hamas.Majina ya mateka yakasomwaWaziri Mkuu huyo wa Israel ameyasoma majina ya mateka ambao bado wako mikononi mwa Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza na pia akaueleza mkutano kuwa amesambaza vipaza sauti au spika katika eneo lote la Gaza ili anapoongea leo, azungumze moja kwa moja na mateka huko walikofichwa. Na hapo akabadilisha lugha na kuongea kwa kihebrania akiwaahidi kuwa atawakomboa. Vilevile amedokeza kuwa kwa namna ya kiintelijensia Israel imefanya simu leo ziweze kusambaza hotuba katika ukanda wa Gaza na hivyo akautumia muda huo kupeleka ujumbe mkali kwa Hamas kuwa ataendelea kuwadhibiti. Bwana Netanyahu pia ameingia ukumbini na vibao viwili vyenye maswali na majibu ya kuchagua japokuwa jibu sahihi kwa mujibu wake na waliojibu kuwa ni All the Above, yaani majibu yote ni sahihi. Maswali yote yalikuwa yakiwatuhumu Iran, Hamas, Al Caeda, Hezbollah na Houthi kuwa pia wanaitakia kifo Marekani na wameua watu wengi Ulaya. Huenda hotuba hii ya Netanyahu ikaingia katika orodha ya hotuba tano ndefu zaidi baada ya ile ya Rais wa Marekani Donald Trump wa Marekani, Ya Mahmoud Abbass wa Palestina na Félix-Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao wote hao walitumia zaidi ya dakika arobaini licha ya muda wa hotuba uliopangwa kuwa angalau dakika 15.
Duration:00:03:54