
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Hali si hali huko El Fasher nchini Sudan, watoto 'walipa gharama' zaidi
10/29/2025
Ghasia zinazoendelea kwa kasi zinawakwamisha zaidi watoto katikati ya mashambulizi ya mabomu yasiyokoma, mapigano makali, na uhaba mkubwa wa chakula, maji salama na dawa kwa zaidi ya siku 500 sasa.“Hakuna mtoto aliye salama,” anasema Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF kupitia taarifa iliyotolewa na makao makuu ya shirika hilo jijini New York, Marekani leo.Taarifa hiyo pia inamnukuu Catherine Russell akisema, “ingawa athari kamili bado haijulikani kutokana na kukatika kwa mawasiliano kote nchini Sudan, inakadiriwa kuwa watoto wapatao 130,000 huko Al Fasher wako katika hatari kubwa ya kukiukwa haki zao, huku kukiripotiwa visa vya utekaji nyara, mauaji na ukataji viungo vya mwili, pamoja na ukatili wa kingono.”Pia kuna taarifa za wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu kukamatwa au kuuawa.UNICEF inatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano, kuhakikisha upatikanaji salama na usiokatizwa wa misaada ya kibinadamu, ulinzi wa raia hasa watoto, na kupatiwa uhakika wa njia salama kwa familia zinazotafuta hifadhi, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Wale wanaohusika na ukiukaji lazima wawajibishwe.Wakati huohuo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limethibitisha kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewataarifu kuwa viongozi wawili wa juu wa WFP nchini wametangazwa kuwa watu wasiotakiwa nchini Sudan na hivyo wameamriwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, bila maelezo yoyote.WFP inaeleza kwamba uamuzi huu wa kuwafukuza Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan na Mratibu wa Dharura wa WFP nchini humo unakuja katika kipindi muhimu kwani mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan hayajawahi kuwa makubwa zaidi kama kipindi hiki, huku zaidi ya watu milioni 24 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na jamii zikikumbwa na baa la njaa.Wakati ambapo WFP na washirika wake wanapaswa kupanua wigo wa msaada, uamuzi huu unalazimisha shirika kubadilisha uongozi bila mpango, jambo linalohatarisha shughuli zinazowaunga mkono mamilioni ya Wasudani walio hatarini kukumbwa na njaa kali, utapiamlo, na hata kifo kutokana na njaa.WFP na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kuzungumza na mamlaka za Sudan kupinga hatua hii na kutaka ufafanuzi wa uamuzi huo.Tags: Sudan, El Fasher, WFP, UNICEF
Duration:00:02:43
Wagonjwa wanaohitaji tiba zaidi Gaza wasafirishwa kupata tiba zaidi Afrika Kusini na kwingineko
10/29/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, limeongoza uhamishwaji wa wagonjwa kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano kwenye ukanda huo.Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, kuelekea Afrika Kusini, Uswisi na kwingineko, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura.Katika hospital iliyojengwa kwa mahema katika eneo la AL-MAWASI, RAFAH kwenye Ukanda wa Gaza wagonjwa wakihudumiwa kila kona watoto kwa wakubwa Miongoni mwao ni Ibrahim Abu Ashiba, mkurugenzi wa filamu ambaye maisha yake yamebadilika ghafla. Anakumbuka wakati alipojeruhiwa. Anasema, "Nilipigwa risasi mara kadhaa, mara moja kwenye kifua, mara moja kwenye bega, mara mbili mkononi. Risasi hizo mbili zilikata mishipa ya neva ya mkono wangu. Sasa siwezi kushika kamera wala kunyoosha mkono wangu kawaida. Ghafla, maisha yangu yote yalisimama."Safari ya kupona kwa Ibrahim inaanzia Afrika Kusini, ambapo amekubaliwa kwenda kupokea matibabu maalum ambapo anasema "Maisha yangu yote yalikuwa yamesimama baada ya kujeruhiwa hadi waliponipigia simu na kunijulishakwamba nitasafiri kwenda Afrika Kusini kwa matibabu. Ilionekana kama nimezaliwa upya."Mgonjwa mwingine katika hospitali hii ni, Maria Al-Shaer, alijeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyokuwa yakiendelea Gaza, huku akipoteza ndugu zake. Mama yake, Raghda Ahmed Al Shaer, anaelezea mateso hayo. "Maria amepoteza baba yake na ndugu zake wote. Alijeruhiwa na kuvunjika mguu, mifupa na kupoteza nyama. Anahitaji upasuaji wa kuwekewa viungo bandia. Maisha yake yamegeuka, hawezi kutembea, na hali yake ya kisaikolojia imeathirika sana."Uhamishwaji huu umeratibiwa na Shirikisho la Chama cha Msalaba Mwekundu Palestina, kwa msaada wa WHO. Dkt. Luca Pigozzi, Mratibu wa Timu ya Dharura ya WHO, anafafanua umuhimu wake."Huu ni uhamishaji wa kwanza wa matibabu tangu kusitishwa kwa mapigano Oktoba 10. Tumejizatiti kuongeza uwezo wetu kusaidia na kuratibu uhamishaji kwa ajili ya matibabu, kwa ushirikiano wa karibu na Shirikisho la chama cha Msalaba Mwekundu la Palestina."Raghda anaeleza matumaini kwa ajili ya binti yake wanapohama kwenda Uswisi. "Wametupigia kutuarifu kwamba Maria amekubaliwa kusafiri kwenda Uswisi kwa matibabu. Tumefurahi sana kwamba atatembea tena, na hali yake ya kisaikolojia itaboreka. Atarudi kuwa Maria wa kawaida kama tuliyemjua."WHO inasisitiza kuwa wagonjwa takriban 15,000 bado wanangojea idhini ya kupata matibabu nje ya Gaza na inatoa wito kwa nchi zote kufungua milango yote za dharura kwa ajili ya uokoaji wa wagonjwa.
Duration:00:03:24
Kimbunga Jamaica, Katibu Mkuu wa UN azungumza
10/29/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati huu Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake, Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha madhara makubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Taarifa hiyo imemnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba “ana wasiwasi mkubwa” na anashikamana na serikali pamoja na wananchi walioathiriwa vibaya na Kimbunga Melissa.”Katibu Mkuu pia “Amewapa pole familia zote za waliopoteza wapendwa wao katika kimbunga hicho na anawatakia majeruhi wote ahueni ya haraka.”Umoja wa Mataifa umeanza kutoa msaada wa dharura, huku timu zake zikiwa tayari mashinani kusaidia kutathmini madhara na kusaidia juhudi za kitaifa. Pia, umetoa dola milioni nne kwa Haiti na vile vile dola milione nne kwa Cuba kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) ili kusaidia jamii kujiandaa na kupunguza madhara ya kimbunga hicho.Taarifa hiyo imesema Umoja wa Mataifa uko tayari “kutuma wahudumu wa ziada kwa muda mfupi na kuzindua maombi ya misaada ya dharura kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu yatakayosababishwa na kimbunga hicho.”Kimbunga Melissa ni miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Karibea, na kinatishia maisha ya mamilioni ya watu kutokana na mafuriko, uharibifu na watu kufurushwa katika makazi yao.
Duration:00:01:38
29 OKTOBA 2025
10/29/2025
Leo jaridani tunamulika kimbunga Melissa huko Karibea, uhamishaji wagonjwa kutoka Gaza kwenda nchi za nje kupata huduma za kigeni na hali tete kwa watoto nchini Sudan. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaAntonio Guterres ameonesha wasiwasi mkubwa wakati Kimbunga Melissa kikiwa miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kurekodiwa katika Bahari ya Atlantiki kinaendelea kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Karibea.Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha athari kubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, limeongoza uhamishwaji wa kwanza wagonjwa kutoka Gaza tangu awamu mpya ya kusitishwa kwa mapigano. Katika muda wa siku mbili, wagonjwa 41 waliokuwa katika hali mbaya pamoja na familia zao 145 wamehamishwa kutoka eneo la mgogoro, huku maelfu zaidi wakiendelea kusubiri matibabu ya dharura. Flora Nducha na taarifa zaidi.Nchini Sudan hususani katika eneo la El Faher kusinimagharibi mwa nchi, hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya kila siku, huku ghasia, njaa, na vizuizi vya utoaji misaada vikiendelea kuathiri mamilioni ya watu wakiwemo watoto waliokwama katika maeneo ya vita. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
Duration:00:09:53
28 OKTOBA 2025
10/28/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mradi wa TANZIE huko Chuo Kikuu Mzumbe, mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania, unaolenga kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa neno la wiki.Mamilioni ya watu nchini Jamaica na katika ukanda wote wa Karibea wanajiandaa kukabiliana na madhara makubwa ya kimbunga Melissa huku Umoja wa Mataifa na washirika wake wakionya kuhusu tishio kubwa na la haraka la kibinadamu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kufuatia kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi mjini El Fasher, jimbo la Darfur Kaskazini, nchini Sudan. Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa tarehe27 Oktoba 2025 kwa saa za New York marekani, Guterres amesema kwa zaidi ya miezi kumi na minane, wakazi wa El Fasher na maeneo ya jirani wamekuwa wakikabiliwa na mateso makubwa huku makundi ya Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yakizingira mji huo.Na hii leo, Ofisi ya Umoja wa Matiafa ya Haki za Binadamu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi nchini Afghanistan wamechapisha waraka wa taarifa kuhusu madhara makubwa ya kina za haki za binadamu yaliyotokana na kusitishwa kwa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan tarehe 29 Septemba hadi tarehe mosi mwezi huu, — hatua ambayo imezidisha changamoto nyingi ambazo tayari zinawakabili wananchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:11:02
Guterres: ASEAN chukueni hatua kukomesha ukatili Myanmar
10/27/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN kuchukua hatua za haraka kumaliza machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, akisisitiza kuwa mgogoro huo si tishio kwa watu wa Myanmar pekee bali pia kwa amani na usalama wa kanda nzima ya Asia ya Kusini Mashariki. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Duration:00:02:47
UNICEF yachukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX nchini Kenya
10/27/2025
Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi
Duration:00:03:02
27 OKTOBA 2025
10/27/2025
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, hali ya kibinadamu nchini Sudan kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, na masuala ya afya nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa dunia na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN kuchukua hatua za haraka kumaliza machafuko ya muda mrefu nchini Myanmar, akisisitiza kuwa mgogoro huo si tishio kwa watu wa Myanmar pekee bali pia kwa amani na usalama wa kanda nzima ya Asia ya Kusini Mashariki.Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, kufuatia kuendelea kwa mapigano makali katika mji wa El Fasher, huko Darfur Kaskazini nchini Sudan. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wa Mastercard Foundation na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko wa MPOX kwa kutoa huduma muhimu za afya na WASH kwa wagonjwa na waliopona, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga (PPEs), vituo vya kusafisha mikono na ujumbe wa mabadiliko ya tabia za kijamii.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:10:00
Sudan: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu El Fasher
10/27/2025
Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ripoti za vifo vya raia na wimbi la wakimbizi wa ndani, kufuatia kuendelea kwa mapigano makali katika mji wa El Fasher, huko Darfur Kaskazini nchini Sudan. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
Duration:00:02:15
UN80: Umoja wa Mataifa ni nini?
10/24/2025
Msikilizaji, bila shaka umeyasikia mengi kuhusu Umoja wa Mataifa, lakini Umoja wa Mataifa ni nini hasa? Japo kwa ufupi, Anold Kayanda anakufahamisha akianza na historia.
Duration:00:02:17
Siku ya UN ni ukumbusho wa wajibu wetu kuendelea maono ya shirika hilo
10/24/2025
Leo ni Siku ya Umoja wa Mataifa, ikitukumbusha kuanzishwa kwake tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka 1945. Maudhui ya mwaka huu ni "Miaka 80 ya Umoja wa Mataifa: Kujenga Mustakabali Wetu kwa Pamoja - Ishara ya Matumaini kwa ushirikiano wa Kimataifa." Katika kumulika hili, Sabrina Saidi wa idhaa hii amezungumza na mwakilishi wa vijana pamoja na mmoja wa watumishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu maadhimisho ya siku hii, huko jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.
Duration:00:02:10
24 OKTOBA 2025
10/24/2025
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1945.Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ni miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1945, lakini pia ni kumbukizi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikuwa ni tukio la kihistoria na la kukumbukwa. Akiwahutubia wajumbe wa Baraza hilo kwa njia ya mtandao katika kikao cha kumbukizi hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa mageuzi ya dharura na mwamko mpya wa uwajibikaji, akiwakumbusha jukumu lao kuu la kulinda amani ya dunia.Tukiendelea na Siku ya Umoja wa Mataifa, ikitukumbusha kuanzishwa kwake tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka 1945. Maudhui ya mwaka huu ni "Miaka 80 ya Umoja wa Mataifa: Kujenga Mustakabali Wetu kwa Pamoja - Ishara ya Matumaini kwa ushirikiano wa Kimataifa." Katika kumulika hili, Sabrina Saidi wa idhaa hii amezungumza na mwakilishi wa vijana pamoja na mmoja wa watumishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu maadhimisho ya siku hii, huko jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.Msikilizaji, bila shaka umeyasikia mengi kuhusu Umoja wa Mataifa, lakini Umoja wa Mataifa ni nini hasa? Japo kwa ufupi, Anold Kayanda anakufahamisha akianza na historia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:09:56
Baraza la Usalama mna wajibu wa kutimiza ahadi ya kuanzishwa kwa UN - Guterres
10/24/2025
Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ni miaka 80 tangu kuanzishwa kwake 1945, lakini pia ni kumbukizi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikuwa ni tukio la kihistoria na la kukumbukwa. Akiwahutubia wajumbe wa Baraza hilo kwa njia ya mtandao katika kikao cha kumbukizi hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa mageuzi ya dharura na mwamko mpya wa uwajibikaji, akiwakumbusha jukumu lao kuu la kulinda amani ya dunia. Flora Nducha amefuatilia kikao hicho cha maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa na kutuandalia tarifa hii.
Duration:00:03:13
23 OKTOBA 2025
10/23/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Umoja wa Mataifa na tutasikia kutoka mashinani wananchi na asasi za kiraia zina yapi ya kusema kuhusu shirika hili kubwa na la kipekee linalounganisha nchi wanachama 193 duniani.Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la Kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa dharura kwa dunia kuchukua hatua mara moja kukabiliana na janga la kibinadamu linaloongezeka nchini Sudan. Zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada, nchini humo wakiwemo watoto milioni 15 na wakimbizi karibu milioni moja.Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) jana Oktoba 22 ilisema Israeli lazima itimize majukumu yake kama “anayekalia kimabavu” kwa kuhakikisha kuwa msaada unaweza kupita bila vizuizi na kwa kuheshimu haki za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu yanayofanya kazi katika Ardhi ya Palestina Iliyokaliwa kwa Mabavu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea maoni hayo ya ICJ kuwa “muhimu sana,” akiongeza kuwa yametolewa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unafanya kila juhudi kuongeza kasi ya misaada kuingia Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano.Nchini Kenya, wahudumu wa afya waliokuwa wakisubiri hadi siku 15 kupata malipo sasa wanapokea pesa ndani ya saa 72 pekee, shukrani kwa mfumo mpya wa malipo ya kidijitali uliotolewa na Shirika la Sfya la Umoja wa Mataifa WHO na Wizara ya Afya ya nchi hiyo. Mfumo huu unapeleka fedha moja kwa moja kwenye pochi za simu za wafanyakazi, ukipunguza ucheleweshaji, gharama na kuongeza motisha. Wafanyakazi zaidi ya 120,000 sasa wanafaidika, kuboresha ufanisi wa kampeni za chanjo na juhudi za kudhibiti polio.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:15:53
Tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo ni lazima kwa kila mtu - Guterres
10/22/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali. Flora Nducha na taarifa zaidi
Duration:00:02:42
UNMISS yasaidia katika utoaji wa elimu ya uraia nchini Sudan Kusini
10/22/2025
Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi. Leah Mushi anatuletea taarifa ikiangazia namna Sudan Kusini inavyojiandaa na uchaguzi wake mkuu mwakani 2026.
Duration:00:03:34
22 OKTOBA 2025
10/22/2025
Hii leo jaridani tunaangazia mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga, elimu kuhusu uraia nchini Sudan kusini, na kilimo endelevu na vijana nchini Rwanda.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mifumo ya tahadhari za mapema dhidi ya majanga si chaguo tena, bali ni lazima kwa kila mtu duniani, akisisitiza kuwa hatua hizo zinaokoa maisha na mali.Kuanzia furaha ya uhuru hadi maumivu ya kurejea kwa mzozo, safari ya amani ya kudumu Sudan Kusini imekuwa ndefu na bado inaendelea. Licha ya changamoto hizo, matumaini bado ni makubwa miongoni mwa jamii nchini kote kwamba uchaguzi wa amani, huru na wa haki utaleta usalama uliotafutwa kwa muda mrefu pamoja na fursa za maendeleo na ukuaji wa uchumi.Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:11:18
IFAD imewasaidia wanawake wakulima Rwanda kupata ajira na kuimarisha maisha
10/22/2025
Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na jamii za vijijini. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) inahakikisha zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wa miradi yake ni wanawake, kwa lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini. Kupitia mafunzo, huduma za kifedha, na upatikanaji wa masoko, wanawake wanawezeshwa kiuchumi na kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kufuta pengo la kijinsia katika kilimo kunaweza kuongeza pato la dunia kwa asilimia 1. Nchini Rwanda, miradi kama R-YES imewezesha wanawake vijana kuanzisha biashara za kilimo na kutoa ajira. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.
Duration:00:03:12
“NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
10/21/2025
Leo mchambuzi ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
Duration:00:00:54
21 OKTOBA 2025
10/21/2025
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea-Gaza Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP lasema usitishaji wa mapigano umeleta afueni kwa wakaazi kwani sasa misaada inaendelea kuwafikia wenye uhitaji-Naibu Mratibu wa Misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amekuwa ziarani Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na kujionea hali halisi ya wakimbizi, wakimbizi wa ndani na msaada wa kibinadamu-Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa leo limesema katika tathimini yake kuwa ukataji wa misitu umepungua duniani kote ingawa bado kuna shinikizo na hatua zaidi zahitajika-Katika mada kwa kina tunakupeleka nchini Tanzania ambako Vyuo Vikuu vinachukua hatua ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan lile namba 17 la ubia kupitia umataifishaji. -Na kwenye jifunze Kiswahili unapata ufafanuzi wa methali " “NG'OMBE WA MNYONGE HAZAI"
Duration:00:13:03