Jua Haki Zako-logo

Jua Haki Zako

RFI

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Location:

United States

Networks:

RFI

Description:

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Language:

Swahili


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?

5/9/2024
Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume. Wajiku Maina raia kutoka nchini Kenya, anasema katika jamii ya leo hakuna anayeshughulikia haki na majukumu ya mtoto wa kiume, hali ambayo imechangia kizazi kizembe cha mtoto wa kiume. Skiza makala haya kufahamu suluhu kwa baadhi ya changamoto za mtoto wa kiume.

Duration:00:09:54

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023

5/2/2024
Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi. Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika. Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya. Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

Duration:00:09:56

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

4/25/2024
Unamkumbuka kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya. Baada ya takriban mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki. Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi. Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi Katika haya mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa

Duration:00:09:51

Ask host to enable sharing for playback control

Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua

4/17/2024
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi. Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao. Makala haya yameandiliwa na Benson Wakoli Soma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

Duration:00:09:09

Ask host to enable sharing for playback control

Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao

4/16/2024
Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.

Duration:00:09:29

Ask host to enable sharing for playback control

DRC : Jamii ya mbilikimo yalilia serikali kuwapa nafasi kuhudumu serikalini

4/10/2024
Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC. Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali. Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto. Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.

Duration:00:10:05

Ask host to enable sharing for playback control

Haki za raia wa mataifa ya Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya ughaibuni.

4/4/2024
Raia wa mataifa tofauti tofauti ya Afrika ikiwemo Kenya na Uganda huelekea katika mataifa ya kiarabu kutafta ajira Kila mwaka . Changamoto nyingi zikiripotiwa.Kwenye makala haya Florence amezungumza nao wakina dada wanaofanya kazi huko .

Duration:00:10:08

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya : Dhuluma za kijinsia na mrundiko wa kesi mahakamani

3/19/2024
Katika makala haya tujahadili dhuluma za kijinsia swala ambalo limekuwa ni donda sugu kwenye familia zetu, na jamii kwa ujumla. Wakili Latifa Njoki na wakili Elizabeth Njambi wote kutoka nchini Kenya wanafafanua swala la mrundiko wa kesi mahakani zinazohusiana na dhuluma za kijinsia na suluhu.

Duration:00:10:07

Ask host to enable sharing for playback control

DRC: Waasi wa CODECO wadaiwa kutekeleza mauwaji ya kikabila

3/15/2024
Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi. Makundi haya ni yale ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" . Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika raia wakiwa hai. Makala haya yamlika hali wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia 800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .

Duration:00:10:07

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya: siku ya wanawake duniani nini Kipya?

3/8/2024
Siku ya wanawake duniani huadimishwa kila kila tarehe nane ya mwezi machi, kuangazia mchango wa mwanamke katika jamii na pia changamoto zinazowakumba wanawake. Kauli mbiu ya maadimisho ya mwaka huu, nchini Kenya ni uwekeza kwa wanawake ili kufanikisha maendeleo kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

Duration:00:09:17

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya : Wasanii walilia haki yao

3/2/2024
Muungano wa wanamziki nchini Kenya (MAAK), unamtaka mwenyekiti wa Shirika la Hakimiliki ya Muziki ya Kenya, Ezekiel Mutua kujiuzulu kutokana na kile wanadai amekuwa akipora peza za wamziki. Kupitia taarifa muungano huo, unasema Mutua amekuwa akijilimbikizia pesa za wasanii huku wahusika wakiendelea kusalia maskini. Ili kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

Haki ya kutali Africa bila vikwazo

2/21/2024
Ni vigumu kwa watu wachache kutumia usafiri wa beskeli hapa Africa lakini Yusufu raia wa Morocco kwake kutali Africa kwa kuendesha beskeli ni kama kazi. Benson Wakoli aliketi chini na Yusuf, kuthamini safarizake barani Africa na jinsi gani amekuwa akipokelewa na raia wa mataifa mengine.

Duration:00:10:11

Ask host to enable sharing for playback control

Valentine : Haki ya wanaume na wanawake

2/17/2024
Kila mwaka Feb 12 dunia huadimisha siku ya wapendanao, raia wengine wakionesha mapenzi kwa wachumba, pamoja na marafiki. Lakini nini maana ya valentine? kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duration:00:09:56

Ask host to enable sharing for playback control

Kenya : Viongozi wa dini wapinga ushoga

2/9/2024
Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya. Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za kiafrica. Kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duration:00:10:00

Ask host to enable sharing for playback control

DRC : Je haki za raia zilikiukwa kipindi cha uchaguzi?

2/3/2024
Katika makala haya tunapiga darubini kuangazia haki za raia wa DRC wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi, na baada ya uchaguzi. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mapendo Kusudi alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mwandishi wetu Benson Wakoli. Kufahamu zaidi skiza makala haya.

Duration:00:10:00

Ask host to enable sharing for playback control

Haki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

1/26/2024
Katika haya tunaangazia haki ya watoto kupata elimu ambapo utaskia kwa wadau mbalimbali walioazisha kutuo cha elimu cha Fizi kinatoa elimu ya somo la kifaransa nchini Kenya kwa watoto wakimbizi kutoka nchini DRC , Rwanda na Burundi. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2014 lengo likiwa kuwasaidia watoto wakimbikizi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ili kuendelea kujifunza na kuendeleza tamaduni ya lugha ya Kifaransa,hasa ikizingatiwa kwamba nchini Kenya raia wengi huzungumza kingereza na Kiswahili.

Duration:00:10:00

Ask host to enable sharing for playback control

Human watch yatahumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kusadia Sudan

1/21/2024
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kushughulikia vita vinavyoendelea nchini Sudan. Kwa mjibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo, jamii ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushawishi pande hasimu nchini Sudan Kusitsha vita. Ili Kufahamu negi zaidi skiza makala haya.

Duration:00:10:00

Ask host to enable sharing for playback control

Hali ya haki za binadamu nchini Kenya na Tanzania

1/9/2024
Visa vya raia kupotea na kisha kuonekana baada ya siku kadhaa nchini Kenya si vipya tena, hili likishuhudia mara kwa mara nchini Kenya, polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye visa hivi lakini je tume ya haki za binadamu nchini Kenya inafahamu hili? na je nchini Tanzania hali ya hali za haki za binadamu ipo je? Maswali haya yanajibiwa ndani ya makala.

Duration:00:09:46

Ask host to enable sharing for playback control

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha

12/19/2023
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu. Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea. Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC. Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.

Duration:00:09:57

Ask host to enable sharing for playback control

Ipo siku watu wanaoishi na walemavu watapata nafasi sawa katika jamii

12/11/2023
Tarehe 3 Disemba mwaka huu, dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu. Siku hii iliasisiwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa. Nchini Kenya, siku hii ilifana sana huku sherehe ikiandaliwa katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Dagoreti, jijini Nairobi, tulikutana na Grace Wanjiku Maina ambaye alizaliwa na ulimavu lakini amejizatiti na kufanikiwa sana katika Jamii. Licha ya kuishi na Ulemavu Grace ni mshinda wa tuzo ya urembo ya kinadada wanaotumia vitu vya magurudumu, tuzo alioyoishinda 2017 na 2018, vile vile ni mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Dagoreti na pia mkurugenzi katika wakfu wa Sweet Aroma foundation, wakfu ambao unawatetea walemavu. Katika makala ya leo nimeanza kwa kumuuliza, nini kimebadilika tangu aliposhinda taji la urembo la miss Wheelchair miaka 6 iliyopita?

Duration:00:10:05