Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

5/3/2024
Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.

Duration:00:03:13

Ask host to enable sharing for playback control

Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

5/3/2024
Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Matal Amin iliyoko Baidoa nchini Somalia zaidi ya wananchi 1500 wanahaha huku na kule kurekebisha maturubai yao ambayo hasa ndio makazi yao ikiwa ni maandalizi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza muda wowote. Hali ni hivyo hivyo pia katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rama cade kama anavyotueleza Kiongozi wa kambi hiyo Abdulkadir Adinur Aden anasema “Tunajiandaa na msimu wa mvua ili kupunguza athari za mafuriko, tunatumia maturubai ya plastiki kufunika makazi yetu na pia tunatumia viroba vilivyojazwa michanga ili kuzuia mnomonyoko mafuriko yatakapo tukumba.”Wadau mbalimbali wa misaada ya kibinadamu ikiwemo OCHA wamepeleka katika kambi hizo misaada kama vile chakula na lishe, viroba vilivyojazwa michanga, maji safi na salama pamoja na dawa mbalimbali ikiwemo za kipindupindu hata hivyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa OCHA nchini Somalia Erich Ogoso anasema mengi ya makazi hayataweza kuhimili mvua kubwa na hivyo yataharibiwa.“Wananchi wanaoishi katika kambi hii ya Matal Amin walifika hapa mwaka 2017 wakitokea katika mkoa wa Bay ambako walikimbia ukame, mzozo, na mambo mengine. Wamekuwa wakiishi hapa tangu kipindi hicho, mafuriko yanapokuja wamekuwa wakiondoka eneo hili na kukikauka wanarejea na sasa wanajiandaa tena na mafuriko na kuna uwezekano wakutakiwa kuondoka eneo hili.” OCHA wanasema taarifa walizopokea kutoka kwa wadau wao walioko mashinani mpaka kufikia tarehe 28 mwezi Aprili mwaka huu, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Somalia zimewaathiri zaidi ya watu 124,155 na kuwaacha zaidi ya 5,130 bila makazi huku vifo vya watoto saba vikiripotiwa.

Duration:00:02:17

Ask host to enable sharing for playback control

03 MEI 2024

5/3/2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira. Pia tunakupeleka nchini Somalia na Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo, kulikoni? Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika makala tukisalia na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, namkaribisha Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.Na mashinani tutaeleke nchini Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo kufuatili jinsi ambavyo mashirika wanavyohaha kusaidia waathirika wa miozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu

Duration:00:11:11

Ask host to enable sharing for playback control

UN: Wanahabari wana jukumu muhimu la kuelimisha juu ya mabadiliko ya tabianchi

5/3/2024
Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka huu ikibeba maudhui “Vyombo vya Habari kwa ajili ya Sayari: Uandishi wa habari katika kukabiliana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi” kwani Umoja wa Mataifa unasema mchango wa wanahabari na vyombo vya habari ni kiini katika kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu changamoto hiyo ya tabianchi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisistiza kuhusu maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu katika ujumbe wake amesema dunia hivi sasa inapitia dhadhura ya mazingira ambayo haijawahi kushuhudiwa na inatishia kizazi hiki na vijavyo hivyo watu wanahitaji kujua kuhusu janga hili akiongeza kuwa “Waandishi wa habari na wafanyakzi wa vyombo vya habari wana jukumu muhimu la kuwahabarisha na kuwaelimisha. Vyombo vya habari vya kijamii, kitaifa na kimataifa vinaweza kutangaza habari kuhusu janga la mabadiliko ya tabianchi, kupotza kwa bayoanuwai na haki ya mazingira.”Zaidi ya hapo amesema wanatoa ushahidi kuhusu uharibifu wa mazingira ambao unaweza kusaidia kuwawajibisha wahusika na ndio maana haishangazi kwamba baadhi ya watu wenye nguvu, makampuni na taasisi wanafanya kila wawezalo kuwazuia waandishi wa habari za mazingira kufanya kazi yao.Guterres ameonya kwamba hivi sasa “Uhuru wa vyombo vya habari umebinywa. Na uandishi wa habari za mazingira ni taaluma inayozidi kuwa hatari. Makumi ya waandishi wa habari wanaoripoti uchimbaji haramu wa madini, ukataji miti, ujangili na masuala mengine ya mazingira wameuawa katika miongo ya hivi karibuni nakatika idadi kubwa ya kesi zao, hakuna mtu ambaye amewajibishwa.”Akiunga mkono kauli hiyo mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Audrey Azoulay amesema “Wakati ubinadamu unakabiliana na hatari hii iliyopo, lazima tukumbuke, katika Siku hii ya Dunia, kwamba changamoto ya mabadiliko ya tabianchi pia ni changamoto ya uandishi wa habari na wanahabari. Hakuna hatua madhubuti ya hali ya hewa inayowezekana kufikiwa bila fursa huru ya kupata habari za kisayansi na za kuaminika. Ndiyo maana maudhui ya mwaka huu yanaangazia uhusiano muhimu kati ya kulinda uhuru wa kujieleza ambayo ni manufaa ya umma duniani na kulinda sayari yetu.”Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO ya hivi karibuni kabisa katika miaka 15 iliyopita kumekuwa na mashambulizi 750 dhidi ya wanahabari na vyombo vya habari vinavyoripoti masuala ya mazingira na mashambulizi hayo yanaongezeka.Na zaidi ya hayo “Asilimia 70 ya waandishi wa habari za mazingira wamekuwa waathiriwa wa mashambulizi, vitisho au shinikizo kwa sababu ya kazi yao, na waandishi wa habari za mazingira 44 wameuawa katika miaka hiyo 15 iliyopita. Hivyo Bi. Azoulay amesisitiza kuwa “Upatikanaji wa habari za kuaminika ni muhimu zaidi katika mwaka huu wa chaguzi kuu ambapo wananchi wapatao bilioni 2.6 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kushiriki haki yao ya msingi ya kupiga kura.”Hivyo Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba “Bila ukweli, hatuwezi kupigana na habari potofu na za uongo. Bila uwajibikaji, hatutakuwa na sera madhubuti na bila uhuru wa vyombo vya habari, hatutakuwa na uhuru wowote hivyo uhuru wa vyombo vya habari sio chaguo, bali ni lazima.”Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametoa wito kwa serikali, sekta binafsi na mashirika ya kiraia kuungana na Umoja wa Mataifa katika kuthibitisha dhamira ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari na haki za wanahabari na wanataaluma wa vyombo vya habari duniani kote.

Duration:00:02:23

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"

5/2/2024
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."

Duration:00:00:53

Ask host to enable sharing for playback control

02 MEI 2024

5/2/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Nchini Kenya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameathiri maelfu ya watu yakisababisha vifo na kuwaacha wengi bila makazi. Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirikaRipoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi ESCWA inasema vita inayoendelea Gaza imesababisha athari mbaya za kiuchumi na maendeleo ya binadamu katika eneo zima la Palestina.Niger mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 na ongezeko hili na wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno ELEKEZA NA ELEZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:11:16

Ask host to enable sharing for playback control

Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne

5/1/2024
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi. Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).

Duration:00:02:49

Ask host to enable sharing for playback control

UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano

5/1/2024
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP ambapo kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana” Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi, na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia mashambulizi yanayoendelea likisema“kumekuwa na zaidi ya mashambulizi 360 kwenye vituo vyake tangu kuanza kwa vita. Mbali na makumi ya maelfu ya waathiriwa, miundombinu muhimu imeathiriwa pia, pamoja na kisima cha maji cha shirika hilo kilichoko katika jiji la Khan Younis.”Na ili kukarabati chanzo hicho cha maji UNRWA inasema kunahitajika kuondoa tani za uchafu ikiwemo vilipuzi na vifaa vingie vya mabaki ya virta kama vilivyobainiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada wa kutegua mabomu UNMAS nav yote vinahitaji kuondolewa kwa usalama kipande kwa kipande,."Na wizara ya afya ya Gaza imeonya kwamba endapo hakutopatikana usitishwaji mapigano basi Maisha ya watu yataendelea kukatiliwa zaidi na hali itakuwa janga kubwa la kibinadamu kwani hadi sasa takriban watu 34,568 wameuawa na 77,765 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7 mwaka jana.

Duration:00:01:57

Ask host to enable sharing for playback control

01 MEI 2024

5/1/2024
Hii leo jaridani inaangazia hali ya kibinadamu Rafah ambapo wakimbizi wa ndani Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano. Pia inamulika udhibiti wa taka za plastiki kambini Kakuma. Makala inaangazia jamii ya watu wa asili na mashinani inatupeleka nchini DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, ambapo mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Makala inaangazia changamoto za mabadiliko ya tabianchi zilizowalazimisha wanawake wa jamii ya Kimaasai nchini Kenya kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na athari hizo ili kujikimu kimaisha.Na katika mashinani inayotupeleka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Goma Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo vurugu za kutumia silaha zinaendelea kusababisha raia kupoteza maisha yao. Katika video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi DRC, wanawake wanaomba amani irejee.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka

5/1/2024
Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Ninapoona plastiki naona fursa za ajira! Ni kauli hiyo ya Raphael Bassemi, mkimbizi kutoka DRC akiwa hapa kambini Kakuma akizungumza huku wanawake na wanaume waliovalia maovaroli na glovu na barakoa wakiokota taka. Anasema anafurahi anapoona jamii inashiriki na zaidi ya yote wanawake wasiokuwa na ajira sasa wameajiriwa, "Nilipoanza nilijikita tu kwenye plastiki, lakini ilibainika kuwa kuna takangumu nyingi za kudhibitiwa. Sasa ninajishughulisha na aina zote za taka.”Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaonesha taka mbalimbali zikiwemo mifupa ya mafuvu ya ng’ombe, vyuma, seng’eng’e na kadhalika. Sasa amesharejeleza tani zipatazo 100 za takangumu."Tunatengeneza rula kwa ajili ya wanafunzi, vibanio vya kuanikia nguo, sahani za kulia chakula na vikombe vya chai na kahawa. »Raphael na wenzake wakiwa kwenye kiwanda hiki alichoanzisha wanapata ugeni ukiongozwa na Dominique Hyde kutoka UNCHR. Baada ya ziara, Bi. Hyde anasema, "Kilichotuvutia ni jinsi wanaweka mawazo yao kwenye hii biashara ili istawi, na pia kushirikisha jamii ipate ajira na hatimaye kipato walipie elimu na umeme. Kama sisi sote tunahitaji kazi, wao wanahitaji kazi, na wao wameanzisha hii ajira wenyewe. »Sasa Raphael anasema jamii ina furaha naye ana furaha na zaidi ya yote."Ninapoona wanawake ninaofanya nao kazi wana furaha, nami nina furaha na ninatamani kuchukua hatua zaidi."

Duration:00:01:42

Ask host to enable sharing for playback control

Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka

4/30/2024
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki ambao walikuja katika jukwaaa hilo na azimio maalum linalohimiza mama kuvaa kofia yake ili kusaidia kutatua migogoro kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi kimataifa. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili akianza kwa kufafanua kuhusu azimio hilo

Duration:00:08:38

Ask host to enable sharing for playback control

30 APRIL 2024

4/30/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4. Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,"Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linashirikisha wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira kupitia upandaji miti na kupitia video iliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus FM nampisha mwanaharakati wa mazingira ambaye alitembelea eneo Bunge la Ngong katika kaunti ya Kajiado jijini Nairobi ili kushirikiana na wanafunzi katika kutimiza wito wa UNEP wa upanzi wa miti.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:12:36

Ask host to enable sharing for playback control

Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund

4/29/2024
Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Duration:00:03:37

Ask host to enable sharing for playback control

29 APRILI 2024

4/29/2024
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi. Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.Mashinani ikiwa ni wiki ya chanjo, kniniki tembezi inayofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imekuwa uti wa mgongo wa mfumo wa afya nchini Somalia na tunakutana na Jamila Moham, Mhudumu wa afya ya jamii katika kijiji cha Dhusamareeb.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:08

Ask host to enable sharing for playback control

UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza

4/29/2024
Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni. Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhimu kama maji ya kunywa ambapo wakimbizi wa ndani wanapokea chini ya lita moja ya maji kwa mtu kwa ajili ya kunywa, kufua na kuonga ikiwa ni tofauto kubwa na lita 151 ambacho ni kiwango cha chini wanachostahili kupata.Na jana Jumapili UNRWA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada w uteguzi wa mabomu UNMAS walianza operesheni muhimu ya kutathimini uharibifu katika vituo vya UNRWA kuweka alama kwa makombora yoyote na vifaa vyovyote ambavyo hvijalipuka.Mitambo 165 ya UNRWA huko Ukanda wa Gaza imeathiriwa wakati wa vita hii inayoendelea. Na UNMAS inasema ili kuifanya Gaza kuwa salama dhidi ya vifaa vya milipuko ambayo haijalipuka inaweza kuchukua miaka 14.

Duration:00:01:59

Ask host to enable sharing for playback control

Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji

4/29/2024
Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii. Mbinu hii inayoendeshwa na wana jumuiya wenyewe inaweka kiwango kipya cha usaidizi wa kibinadamu nchini humo, kama anavyoeleza Mola Suleiman ambaye ni Mshiriki wa Msaada wa WFP anasema, "Wanaotambua wenye uhitaji zaidi sio viongozi, bali watu wasioegemea upande wowote waliochaguliwa na jamii. Tunaweza kwenda kwenye madawati ya usaidizi yaliyoanzishwa huko wilayani Kebeles na viunga vyake na kupeleka malalamiko yetu. Kwa kufuata utaratibu wa uwazi, tunakagua na kuthibitisha wale waliochaguliwa na jumuiya pana, kwakweli huu mfumo ni bora kuliko ule wa awali”Selam Ambachew ni mwanakamati aliyechaguliwa na jamii."Kama jumuiya, tulichagua kamati, kisha kamati ikaanza tathmini yake, tunapokea orodha ya watu wote wanaoishi katika eneo hili, na tunachunguza orodha ili kuona ni nani anayefaa kwa vigezo vya usaidizi katika jamii"Tadel Gebeyehu ni mmoja wa wananchi walionufaika na mfumo huu mpya wa jamii yenyewe kuchagua wenye uhitaji zaidi wa Msaada wa kibinadamu, anasema "Tulipewa kadi za mgao na lazima tuzioneshe tunapokwenda kupokea chakula. Kadi hizi za mgawo ni muhimu kwa sababu zinazuia watu masikini kunyanyaswa"Ama hakika mwitikio wa kibinadamu nchini Ethiopia unazingatia uwazi, unaendeshwa kwa kuzingatia takwimu na kufikia wale wenye uhitaji zaidi, na hili linathibitishwa Haftom Gebretsadik mmoja wa wagawaji wa msaada.“Mchakato wa kugawa Msaada ni mzuri sana, kila nyanja ni nzuri sana, kinachofanya uwe ya kipekee ni heshima ya utu na ubinadamu. Mfumo ni wa uwazi, hakuna mkanganyiko wala wizi, kwa ujumla mchakato huo ni wa kupongezwa”.

Duration:00:02:28

Ask host to enable sharing for playback control

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika migogoro katika jamii za asili - Alois Porokwa

4/26/2024
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili iliyopita lilipewa kipaumbele cha juu wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 jijini Nairobi, Kenya. Wakati huo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.

Duration:00:04:03

Ask host to enable sharing for playback control

Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF

4/26/2024
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.

Duration:00:02:11

Ask host to enable sharing for playback control

26 APRILI 2024

4/26/2024
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo nchini Sudan, na jinsi amabvyo mzozo huo unavyathiri wanawake. Makala tunaangazia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za watu wa asili na mashinani usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi nchini Kenya. Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.Na tukisalia nchini Sudan, mwaka mmoja wa mzozo umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Katika makala Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanahaha kushughulikia changamoto za usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:12:08

Ask host to enable sharing for playback control

Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan

4/26/2024
Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Fatima sio jina lake halisi, tunalitumia hili ili kuficha utambulisho wake na hapa anaanza kueleza yale yaliyomsibu akiwa mikononi mwa wanamgambo wenye silaha.“Nilibakwa mara tatu. Aliniambia lala chini, usipotaka kulala chini naweza kukuuwa. Sijui sasa kama ni huyo mwanaume aliniingilia mara tatu au kulikuwa na wengine.” Akiwa na kiwewe na aliyekata tamaa, Fatima akaukimbia mji wake wa Khartoum akiwa na watoto wake kwenda kusini mashariki mwa Sudan, kusaka hifadhi na alipofika huko, anasema “Nilikwenda kuripoti tukio hilo katika kliniki na kusaka msaada ili waweze kunifanyia uchunguzi wa jumla. Nikaenda hospitalini na kila kitu kilikuwa sawa. Baada ya miezi miwili nilienda tena kliniki na wafagundua kuwa nina ujauzito.”Pole sana Fatima, sasa ni nini unachohitaji wakati huu nchi yako bado ingali vitani? “Tunahitaji amani kwa ajili yetu, ili tuweze kurudi na kuishi nchini Sudan.”Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama vile UN WOMEN, OCHA, UNHCR na hata Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili wa Kingono kwenye mizozo wamekuwa wakipazia unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudan huku wakieleza wasiwasi wao mkubwa kuwa ukubwa halisi wa mgogoro bado haujajulikana na kumekuwa na viwango vidogo vya kuripoti matukio ya kikatili kwani baadhi ya wanawake na wasichana wanaogopa unyanyapaa na kutokuwa na imani na taasisi za kitaifa.

Duration:00:02:02